Riwaya ya Uhuru wa watumwa katika muktadha wa simulizi za watumwa
Loading...
Date
2011
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Tasinifu hii imeichambua riwaya ya Uhuru wa watumwa katika muktadha simulizi za watumwa. Data na taarifa za utafiti zilikusanywa kutoka maktabani na uwandani, na mbinu zilizotumika kukusanyia data ni mbinu ya uchambuzi matini iliyotumika kutupatia data za msingi na data za upili, na mbinu ya mahojiano iliyotupatia data nyongeza za msingi. Nadharia ya Naratolojia imetoa mwongozo katika uchambuzi wa simulizi tatu teule za watumwa na kubaini ruwaza na motifu za simulizi za watumwa. Imebainika kuwa simulizi hizo zina ruwaza ya; kutiwa utumwani,mateso na hali ngumu utumwani, kupatikana kwa uhuru na maisha baada ya uhuru. Baadhi ya motifu zilizojadiliwa katika simulizi hizo ni motifu ya safari, motifu ya ukatili wa wamiliki watumwa, motifu ya kujaribu kutoroka bila mafanikio na motifu ya kubadili majina. Hali hii imedhihirisha kuwa simulizi hizo zinafanana kwa kiasi kikubwa kifani na kimaudhui. Uchambuzi wa riwaya ya Uhuru wa Watuniwa umetanyika kwa kulinganishwa tto ruwaza na motifu za simulizi teule za watumwa. Wilda ya uchambuti imebainika kuwa riwaya hii inahusiana kwa kiasi kikubwa na simulizi teule la watumwa kifani na kimaudhui. Tofauti ndogo ndogo zilizojitokeza zimejadiliwa pia. Mwisho limetolewa hitimisho la utafiti mzima pamoja na mapendekezo ya maeneo yanayohitaji kutafitiwa zaidi iii kuweza kukuza uwanja wa simulizi za watumwa za Kiswahili na fasihi ya Kiswahili kwa ujumla.
Description
Available in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library (THS EAF PL8704.M38H46)
Keywords
Swahili language, Uhuru wa watumwa
Citation
Henry, Grace (2011) Riwaya ya Uhuru wa watumwa katika muktadha wa simulizi za watumwa,Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam