Muundo na dhima ya vielezi katika kiswahili

dc.contributor.authorAmanzi, Mussa Omari
dc.date.accessioned2021-08-04T13:03:10Z
dc.date.available2021-08-04T13:03:10Z
dc.date.issued2016
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr.Wilbert Chagula Library, class mark (THS EAF PL8702.A52)en_US
dc.description.abstractTasinifu hii ni Matokeo ya utafiti ulioshughulikia muundo na dhima ya vielezi katika Kiswahili na imegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia tatizo la utafiti na kiunzi cha nadharia kilichotumika katika uchambuzi wa mada. Sura ya pili imefanya mapitio ya maandiko mbalimbali yaliyoibua utafiti huu.sura ya tatu imefafanua mbinu anuwai zilizotumika kuendesha utafiti huu, sura ya nne imejihusisha na uchanganuzi wa data ulioibua mchango mpya wa utafiti huu ambapo sura ya mwisho imefunga mjadala kwa kutoa muhtasari wa tasinifu nzima na ushauri kwa utafiti mwingine unaonekana na utafiti huu. Matokeo y a utafiti huu yanaonesha kuwa, kimofolojia, vielezi vya Kiswahili vinaweza kuundwa kwa kuongeza(ki-) mwaanzoni mwa baadhi ya nomino au vivumishi; kuongeza (ku-) mwanzoni mwa baadhi ya vimilikishi; kuongeza (vi-) mwanzoni mwa baadhi ya vivumishi; kuongeza kiangami (-ni) mwishoni mwa baadhi ya nomino za muelekeo na baadhi ya maneno yasiyo na kategoria yoyote (vieleziasilia/ushadidi). Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa kisintaksia , baadhi ya mafungu ya maneno hufanya kazi za uelezi kamavile kirai elezi ambacho kinaweza kuundwa na kielezi peke yake; kielezi zaidi ya kimoja; mfano E + E,(anakula vizuri sana), E + E + E, ( anampiga paka sokoni asubuhi mapema); kielezi pamoja na kihusishi E + H , (anachuma maua juu ya mti) E + E + H, (anafundisha somo vizuri sana mbele ya darasa); kirai husishi elezi (anacheza mpira kwa madaha), pia, kishazi elezi ambacho huundwa kwa kuanza na maneno ya viunganishi vinavyounganisha sentensi zaidi ya moja ndani ya sentensi moja, ambavyo vinachanuza utegemezi 9kishazi tegemezi), kama vile japokuwa, ingawa kwa sababu kama na mengine mengi; mfano (juma anakula chakula, ingawa anaumwa tumbo), si hivyo tu, bali kisintaksia, utafiti umeonesha namna ya utokeaji wa vielezi katika tungo za Kiswahili kwa vielezi kuhamahama kwa kuwa mwanzo, kati au mwisho; (N + T+E) N+T+E+N )(E+N+T+N) kuhamahama huku kunategemea zaidi kama vielezi vinaelezea neon tu au sentensi nzima au yambwa lakini hutokea kukaa karibu na kijalizo chake(antecedent) na wakati mwingine hukubali kukaa mwanzoni mwa tungo. Matokeo ya utafiti huu yameonesha pia, kisemantiki, vielezi vina dhima mbalimbali katika tungo za Kiswahili. Dhima kuu ya vielezi ni kueleza zaidi kuhusu kitenzi, kivumishi, kielezina sentensi nzima kwa kukumisha umahali, uwakati, uidadi na unamna. Pia, utafiti umeeleza maana mahususi zinazojitokeza wakati vielezi vinapohamahama kwa kuwa mwanzo, kati au mwisho. Kwa ujumla, vielezi katika lugha ya Kiswahili vina miundo yake maalumu na dhima zinazojipambanua katika lugha ya Kiswahili tu.en_US
dc.identifier.citationAmanzi, M. O (2016) Muundo na dhima ya vielezi katika kiswahili, Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/15312
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Dar es salaamen_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectGrammaren_US
dc.titleMuundo na dhima ya vielezi katika kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Mussa omari amanzi.pdf
Size:
7.17 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: