Usawiri wa mwanamke katika taarab ya mipasho: mfano kutoka nyimbo za mzee Yussuf Mzee
No Thumbnail Available
Date
2013
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza usawiri wa mwanamke katika nyimbo za taarab ya mipasho za Mzee Yussuf Mzee. Malengo mahsusi yalikuwa ni manne nayo ni kubainisha usawiri wa mwanamke katika nyimbo za taarab ya mipasho za Mzee Yussuf, kueleza aina ya usawiri wa mwanamke inayojitokeza zaidi katika nyimbo hizo za taarab ya mipasho za msanii teule, kubainisha sababu zinazofanya mwanamke asawiriwe hivyo na kueleza uhusiano baina ya hadhi aliyopewa mwanamke katika nyimbo za taarab ya mipasho za msanii huyu na hali halisi ya mwanamke wa Tanzania. Nadharia ya Ufeministi ilitumika katika uchambuzi wa data wa tasnifu hii. Mbinu za ukusanyaji wa data maktabani kwa kusoma maandiko na machapisho mbalimbali na uwandani zilitumika katika utafiti huu. Kwa upande wa mbinu za uwandani, tulitumia mbinu ya ushuhudiaji, usaili, hojaji na usikilizaji wa vipindi vya taarab redioni na katika televisheni. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba Mzee Yussuf Mzee anamsawiri mwanamke katika namna mbalimbali kama vile chombo cha starehe cha mwanaume, kiumbe mwenye heshima, mnyenyekevu na mpole, mvumilivu na mwaminifu, mficha siri, mshauri na mlezi wa familia. Kwa ujumla, utafiti wetu umebaini kwamba usawiri wa mwanamke kama chombo cha starehe kwa mwanaume na mwanamke kama pambo ndio unaojitokeza zaidi kuliko aina nyingine ya usawiri. Utafiti wetu umebaini kwamba miongoni mwa mambo yanayofanya msanii amsawiri mwanamke hivyo ni mahitaji ya soko la muziki wa taarab, mapenzi ya Mzee Yussuf kwa wanawake, mwanamke mwenyewe, utamaduni, mila na desturi na utekelezaji dhaifu wa sera za masuala ya jinsia nchini. Pia, utafiti umebaini kwamba hadhi anayopewa mwanamke katika nyimbo za Mzee Yussuf haifanani na mwanamke halisi wa Kitanzania katika jamii.
Description
Kinapatikana Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaa, Idara ya East Africana,
(THS EAF PL8703.5.R35)
Keywords
Swahili literature, Swahili poetry
Citation
Ramadhan, S. K (2013) Usawiri wa mwanamke katika taarab ya mipasho: mfano kutoka nyimbo za mzee Yussuf Mzee, Digrii ya Umahiri katika Kiswahili (M. A. Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.