Uumbaji wa ualbino katika fasihi ya kiswahili: uchambuzi wa kazi teule

dc.contributor.authorMahenge, Elizabeth Godwin
dc.date.accessioned2021-10-06T08:54:08Z
dc.date.available2021-10-06T08:54:08Z
dc.date.issued2019
dc.descriptionAvailable in print form, Eat Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library,(PL8704T34M333)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulihusu uchambuzi wa kazi teule katika fasihi ya kiswahili ili kuona namna uumbaji wa ualbino unavyofanyika. Utafiti ulikuwa na malengo mahususi manne ambayo ni: kubainisha imani zinazoumba ualbino katika kazi teule za fasihi ya Kiswahili; kuchambua jinsi lugha inavyoumba ualbino katika kazi teule za fasihi ya Kiswahili; kuelezea dhima ya msimulizi anayesimulia hadithi ya ualbino katika kazi teule; na kujadili sauti za usimulizi zinazotumiwa kuumba ualbino katika kazi teule. Utafiti ulihusisha kazi nane za fasihi ya Kiswahili ambazo ni: Takadini, Nje Ndani, Zindera, Baba Ne-Musa!,"Mimi Albino", "Wimbo Wangu Albino" "Albino", na "Mauaji ya Albino". Mbinu ya uchambuzi wa nyaraka ilitumika ili kupata matokeo ya utafiti huu. Mbinu hii ya uchambuzi iliongozwa na Nadharia ya Naratolojia. Nadharia hii inahusika kuchunguza namna usimulizi unavyofanywa katika simulizi. Utafiti unafuata mkabala wa Bal ambao unaona kuna usimulizi katika kila kitu. Data zilipatikana baada ya kusoma kwa kina kazi teule pamoja na kufanya mahojiano kwa ajili ya utafiti wa awali wa utafiti huu. Mkabala uliotumika katika uchambuzi wa data ni wa kitaamuli ambao ni wa kimaelezo na uliwezesha kupatikana kwa matokeo ya utafiti huu. Kwanza, utafiti umebaini kuwa kuna imani mbalimbali zinazoelezea asili ya kuzaliwa mtoto mwenye ualbino. Imani hizi zinatokana na visasili vilivyopo katika jamii. Pili, utafiti umebaini kuwa, msimulizi anatumia tamathali za usemi ili kuumba ualbino kiubaguzi na kiunyanyapaa kwa upande mmoja; na pia anatumia tamathali za usemi ili kuumba ualbino kiujumuishwaji kwa upande mwingine. Tatli, utafiti umebaini kuwa msimulizi anajitokeza kwa dhima nne ambazo ni kusimulia, kuwasiliana, kukosoa na kutekeleza itikadi. Katika dhima hizi, msimulizi anaweza kuwa hai (akishiriki katika kusimulia) au tuli (akijitenga kusimulia). Nne, utafiti umebaini kuwa, sauti za usimulizi zinatumika kwa makusudi maalumu ambayo ni ama kuunga mkono jambo fulani au kulipinga. Matumizi ya nafsi ya kwanza na ya pili yanaonesha kuunga mkono jambo; wakati matumizi ya nafsi ya tatu yanaonesha kulipinga. Mapendekezo yanayotolea na utafiti huu ni kufanya utafiti mwingine katika kumbo mahususi za fasihi ili kuona namna ualbino kwa umahususi na ulemavu kwa ujumla unavyoumbwa katika kumbo hizo. Vilevile utafiti unapendekeza Nadharia ya Naratolojia itumiwe zaidi na wachambuzi wa kazi za kifasihi kwa kuwa inamwezesha mchambuzi kuufahamu uhalisia wa simulizi kupitia nafsi mahususi zinazotumika katika kusimulia. Nadharia hii iko karibu na uhalisia.en_US
dc.identifier.citationMahenge, E. G. (2019) Uumbaji wa ualbino katika fasihi ya kiswahili: uchambuzi wa kazi teule.tasnifu ya PhD(kiswahili). Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/15811
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectLanguage and languagesen_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.subjectAlbinos and albinismen_US
dc.subjectTanzaniaen_US
dc.titleUumbaji wa ualbino katika fasihi ya kiswahili: uchambuzi wa kazi teuleen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Elizabeth Godwin Mahenge.pdf
Size:
6.75 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:
Collections