Muundo wa kirai nomino cha Kibena.

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Tasinifu hii ni matokeo ya utafiti ulioshughulikia Muundo wa Kirai Nomino cha Kibena, na imegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia Tatizo la Utafiti na Kiunzi cha Nadharia kilichotumika katika utafiti huu. Sura ya pili imeangazia mapitio mbalimbali ya maandiko yaliyoibua utaflti huu. Sura ya tatu imetalii mbinu anuuai zilizotumika kucndcsha utafiti huu. Sura ya nne imejihusisha na uchanganuzi data ulioibua mchango mpya wa utaflti huu ambapo suu ya mwisho imehitimisha kwa kutoa muhtasari wa tasinifu nzima. Matokeo ya Utafiti huu yanaonyesha kuwa Muundo wa Kirai nomino cha Kibena kwa upande. mmoja una sifa zinazofanana na zile za virai nomino vya lugha nyingine za Kibantu kikiwemo Kiswahili. Miongoni mwa sofa hizo ni pamoja na viandami vinavyounda KN hiya ambavyo ni vibainishi (vimilikishi na vionyeshi) na vikumushi (vivumishi vya sifa na idadi, virai husishi na vishazi rejeshi). Vile vile viandami vingi katika mpangilio wa KN hiyo hutokea kulia kwa neno kuu (nomino). Katika mkururo wa viandami hivyo, kibainishi kimilikishi huliandamia neno kuu, kisha vijenzi vingine hufuata. Si hivyo tu bali pia uamilifu wa KN ya Kibena katika sentensi ni ule unaojibainisha katika lugha nyingine, ukiwa ni kiima cha sentensi, yambwa ya kitenzi, yambiwa, kijalizo cha kihusishi na kikumushi cha kirai nomino, mpangilio wa vijenzi wake, unaoruhusu utokeaji wa kionyeshi kabla ya nomino na hivyo kuwa na mpangilio wa: (B) + N + (B) (KV) (F) (S). Katika KN ya Kibena kuna kiandami de kinachokumusha nomino, kivumishi au kibainishi kionyeshi. lli kufanya hivyo kiandami hiki kinatalii katika maeneo mbalimbali ya kirai hicho. KN ya Kibena pia inaruhusu kutumia ama kutotumia kiambishi awali tangulizi (augment). Kuhusu suala la ubebaji viandami, utafiti umebaini kwamba KN ya Kibena inakubali kuturnia kijenzi kimoja hadi vitano katika mazugumzo ya kawaida. Miundo ya kiuchamko (yenye viandami vingi) inaonekana kuwa ni ya kinadharia tu. Hivyo haitumiki kiuhalisia. Kwa jumla KN ya Kibena ina viandami vinavyofuata na visivyofuata ruwaza maalum zilizobainishwa k"'a kind katika kali hii.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8025.M3256)
Keywords
Bena language, Bantu language, Tanzania
Citation
Mbogela, E. (2011). Muundo wa kirai nomino cha Kibena. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.