Matumizi ya misimu ya vijiweni katika lugha ya Kiswahili : Mifano katika Jiji la Dar es salaam

Loading...
Thumbnail Image
Date
2013
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahus matumizi ya misimu ya vijiweni katika lugha ya Kiswahili, katika mkoa wa Dar es Salaam. Ulichunguza na kueleza misimu mbalimbali ya vijiweni na maana zake, makundi na rika linalopendelea zaidi kutumia misimu na sababu zake na faida na hasara za matumizi ya misimu hiyo. Watafotowa 90 walihojiwa kwa kutumia sampuli nasibu tarbakishi na mbinu za hojaji, mahojiao na ushuhudiaji. Utafiti huu umebaini misimu mbalimbali ya vijiweni inayotumika katika lugha ya Kiswahili na maana zake, makundi na rika linalopendelea zaidi kutumia misimu hiyo na faida na hasara za matumizi ya misimu ya vijiweni katika lugha ya Kiswahili. Mwisho utafiti huu umependekeza kuwa utafiti mwingine wa aina hii ufanyike katika mikoa mingine mbali na Dar es Salaam kwani misimu inatumika sana katka lugha ya Kiswahili kwa nchi nzima, pia kuchunguza vyombo mbalimbali vya habari vinavyotumia misimu ya vijiweni katika utangazaji wao na athari zake katika lugh ya Kiswahili nchini Tanzania, kueleza asili ya misimu ya vijiweni inayotumika katika lugha ya Kiswahili na kuchunguza ni kwa nini watu wenye umri kati ya miaka 31-45 na kuendelea hawatumii misimu ya vijiweni zaidi katika lugha ya Kiswahili nchini Tanzania.
Description
Available in printed form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8702.I27)
Keywords
language and languages, Swahili language, Style
Citation
Ibrahim, A. (2013) Matumizi ya misimu ya vijiweni katika lugha ya Kiswahili : Mifano katika Jiji la Dar es salaam . Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.