Lugha ya uganga na uchawi katika fasihi ya kiswahili ; uchunguzi katika riwaya ya mirathi ya hatari na tamthilia ya ngoma ya ng`wanamalundi

Loading...
Thumbnail Image
Date
2018
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umechunguzwa namna matumizi ya lugha ambacho ni moja kati ya vipengele vya fani kilivyotumiwa na waandishi wa kazi za fasihi ya Kiswahili kujadili uganga na uchawi huku tukirelejelea katika kazi mbili za nathari ambazo ni riwaya ya Mirathi ya Hatari ( 1997 ) na tamthilia ya Ngoma ya Ng’wanamalundi ( 1988 ). Utafiti huu umeongozwa na malengo mahsusu ambayo ni mosi, kubainisha lugha iliyotumika kujadili uganga na uchawi katika kazi teule, pili, kufafanua mchango wa matumizi ya lugha katika kujadili uganga na uchawi katika kazi teule. Utafiti huu ni wa kimaktaba, umefanywa jatika maktaba ziulizopo chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kwa kutumia mbinu ya uchambuzi matini. Data zimechambuliwa kwa mkabala wa kitaamuli kwa kutumia nadharia za semiotiki na Ontolojia ya kibantu. Katika utafiti huu mtafiti amegundua kuwa, lugha hufinywangwa kwa namna mbalimbali kwa kutumia mbinu za kisanii za lugha kutegemeana na jambo msanii alilokusudia kuipelekea jamii husika. Kwa mfano,Watunzi wa kazi teule katika kujadili uganga na uchawi wametumia tafsida, tashihisi,mdokezo, dhihaka, takriri, tashibiha, sitiari, chuku, kejeli, semi na kubadili misimbo, ritifaa, tashititi na meto ni mia. Mbinu hizo zimetumika kujadili uganga na uchawi kifani na kimaudhui kwa mfano, imebainika kuwa kifani mbinu hizo zimetumika kujenga dhihaka, kuibua ucheshi, kutambulisha wahusika, kujenga kejeli, kujenga dhihaka, kuibua ucheshi, kutambulisha wahusika, kujenga kejeli, kujenga taharuki na kujenga taswira na hujenga dhamira. Imebainika kuwa, uganga na uchawi vimejadiliwa kama utamadumi wa kiafrika, kama itikadi, kama falsafa na kama tasnifu. Utafiti huu utasaidia watunzi wa kazi mabalimbali za kifasihi katika kutumia vipengele mabalimbali vya kifani katika kuisawiri jamii barabara. Utawaongoza watafiti wa baadaye katika kutafiti veipengele vingine vya fani kama vile maaandhari na wahusika na namna vipengele hivyo vinavyotumika na wasanii katika kufikisha ujumbe wao kwa jamii waliyokusudia.
Description
Available in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library, class mark ( THS EAF GR530.F726 )
Keywords
Swahili literature, Witchcraft, Focklore, Black ant, Tanzania
Citation
Francis, E ( 2018 ) Lugha ya uganga na uchawi katika fasihi ya kiswahili ; uchunguzi katika riwaya ya mirathi ya hatari na tamthilia ya ngoma ya ng`wanamalundi, Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.