Taswira ya nyoka katika ngano za kisambaa

No Thumbnail Available
Date
2011
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Ingawa wanyama ni miongoni mwa raslimali asilia zinazowafaidisha wanajamii kwa namna tofauti tofauti, bado dhima na nafasi ya raslimali hii haijatambulika na wala haijafanyiwa uchunguzi wa kina. Ili kubaini dhima na nafasi ya wanyama katika jamii, Tasinifu hii imejikita katika kutafiti juu ya Taswira ya nyoka katika ngano za Kisambaa. Mifano iliyotumika katika kuchambua tatizo la utafiti huu imetoka wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga. Ili kuyatimiza malengo ya utafiti husika, Tasinifu imegawanyika katika sura kuu tano. Sura ya kwanza imefafanua na kuweka wazi tatizo la utafiti. Sura ya pili imejihusisha na udurusu wa maandiko yaliyolandana na suala la kiutafiti lilijadiliwa ndani ya Tasinifu hii. Sura ya tatu imejadili mbinu zilizotumika kukusanyia na kuchambulia data husika. Sura ya nne inawasilisha matokeo ya utafiti na sura ya tano inatoa muhtasari wa utafiti pamoja na mapendekezo kwa ajili ya kuboresha utafiti unaohusu ngano na fasihi simulizi kwa jumla. Kwa kutumia mbinu na nyenzo za kisasa kama vile kompyuta, radio, kamera ya kidijitali na kinasa sauti, malengo ya utafiti yalifikiwa na kukidhiwa haja maridhawa. Zana hizi zilitumika katika kukusanyia na kuchambulia data. Aidha, utafiti ulitumia mbinu za uwandani na maktabani. Mbali na mbinu hizi, mtafiti aliongozwa na nadharia za umuundo na umuundo leo. Kwa kutumia mkabala wa kihitoria-jamii uliopendekezwa na Zides (1983) na Bottigheimer (1986), tumejadili dhima na nafasi ya taswira ya nyoka katika ngano. Kutokana na utafiti huu, imebainika kuwa taswira za nyoka katika ngano za Kisambaa zinahusiana na muundo wa mfumo wa ontolojia Kibantu.
Description
Available in print form
Keywords
Swahili literature, Shambala language
Citation
Thomas, R.(2011) Taswira ya nyoka katika ngano za kisambaa, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Avaialble at (http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)