Jinsi nyimbo zinavyomjenga mwanamke wa Kikagulu kimaadili

No Thumbnail Available
Date
2013
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Lengo kuu la tasinifu hii ni kuchunguza jinsi nyimbo zinavyomjenga mwanamke wa Kikagulu kimaadili. Tasinifu hii ina sura sita ambapo sura ya kwanza ni utangulizi kwa ujumla, usuli wa tatizo, tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti na mawanda ya utafiti. Sura ya pili ni mapitio ya maandiko yanayohusu nyimbo, maadili, uchanganuzi wa mfumo wa kijinsia uliochanganuliwa na wataalamu tofauti pamoja na nadharia ya Ufeministi iliyotumika katika utafiti huu. Sura ya tatu inaelezea mbinu na njia zilizotumika katika ukusanyaji wa data, vifaa vya utafiti pamoja na eneo la utafiti. Sura ya nne ni mkusanyiko wa mambo yanayomjenga mwanamke na mwanamume katika kabila la Wakagulu pamoja na kubainisha nafasi ya mwanamke kiuchumi, kisiasa na kijamii. Sura ya tano ni uchambuzi wa dhamira za nyimbo zinazoimbwa na wanawake pamoja na kuchunguza uhusiano wake na sifa za kimaadili zinazotakiwa kwa mwanamke wa Kikagulu. Sura ya sita ni muhtasari wa tasinifu nzima, matokeo ya utafiti, mapendekezo na mwisho ni hitimisho. Matokeo yanaonesha kuwa dhamira zilizojitokeza katika nyimbo zinamjenga mwanamke kimaadili ili aweze kuwa na sifa zinazokubalika katika jamii. Pia kuna uhusiano kati ya dhamira zilizojitokeza kwenye nyimbo na sifa zinazotakiwa kimaadili kwa mwanamke wa Kikagulu. Mwanamke hupewa mafunzo kupitia nyimbo, familia, jamii, unyago, methali, hadithi na ngoma. Nafasi ya mwanamke katika jamii imetokana na mafunzo anayopata kupitia nyimbo ambazo humfanya awe na maadili ingawa mafunzo mengine humfanya akandamizwe kijinsia. Hivyo, jamii haina budi kuendeleza mafunzo ambayo yanamjenga mwanamke kimaadili na kuyapiga vita mafunzo yanayomkandamiza ili aweze kupata fursa sawa katika jamii.
Description
Keywords
Kaguru Language, Bantu language, Songs, Tanzania, Women
Citation
Mageni, M.D (2013) Jinsi nyimbo zinavyomjenga mwanamke wa Kikagulu kimaadili, Tasinifu ya M.A. Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)