Usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya za kiswahili: mkabala linganishi
No Thumbnail Available
Date
2011
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Tasnifu hii inahusu Usawiri wa Wahusika wa Kiume katika Riwaya za Kiswahili, ikitumia mkabala Linganishi. Kazi hii imehusisha riwaya ya Miradi Bubu ya Wazalendo iliyoandikwa na Gabriel Ruhumbika ambaye ni mwandishi wa kiume akilinganishwa na mwandishi wa kike Ndyanao Balisidya katika riwaya ya Shida ili kuona namna waandishi hawa walivyowachora wahusika wa kiume katika riwaya zao. Watafiti waliotangulia kama vile Momanyi, C. (2001) na Balisidya, N. (1982 na 1987) wamechunguza namna wahusika wa kike walivyosawiriwa katika kazi mbalimbali za fasihi hasa katika tamthiliya na ushairi na pia kuchunguza namna jamii zinavyowachukulia wahusika wa kike kama vyanzo vya maovu, wahalifu, vyombo vya starehe kwa wanaume na pia ni tegemezi kwa wanaume. Katika utafiti huu, wahusika wa kiume wamesawiriwa kwa mtazamo hasi na chanya pia. Hii imetokana na ulinganishaji wa mwandishi wa kike Ndyanao Balisidya na mwandishi wa kiume Gabriel Ruhumbika. Mwandishi wa kiume amewasawiri wahusika wa kiume kwa mtazamo hasi zaidi kuliko chanya wakati mwandishi wa kike kawasawiri kwa mtazamo chanya zaidi kuliko hasi. Usawiri wa wahusika hao umetofautiana kulingana na mazingira ya wahusika aliyoyachora mwandishi. Matendo ya wahusika hao wa kiume yalitegemea zaidi mazingira yaliyowazunguka pamoja na wakati. Utafiti huu sura kuu tano: Katika sura ya kwanza kuna usuli wa tatizo, tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti na mipaka ya utafiti. Sura ya pili inahusu mapitio ya machapisho na kiunzi cha nadharia. Sura ya tatu ni mbinu za utafiti. Sura ya nne inachambua data na kuziwasilisha huku ikijenga mjadala. Katika sura ya tano tumeweka muhtasari, hitimisho na mapendekezo kwa tafiti zijazo.
Description
Available in print
Keywords
Swahili literature, Characters and characteristics in literature, Tanzania
Citation
Kanwa, O. (2011) Usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya za kiswahili: mkabala linganishi. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Available at http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/search.aspx