Matatizo ya tafsiri katika ripoti za kitaaluma zinazofasiriwa kutoka kiingereza kwenda kiswahili

No Thumbnail Available
Date
2014
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Unversity of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umechunguza matatizo ya tafsiri katika ripoti za kitaaluma zinazofasiriwa kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili kwa kutumia mifano kutoka tafsiri ya Kijitabu cha Viashiria vya Kijinsia 2010. Utafiti huu umefanyika mkoani Dar es Salaam katika wilaya zote tatu: Kinondoni, Ilala na Temeke. Data ya utafiti huu imepatikana kupitia mbinu ya maktabani, hojaji na usaili. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Aina Matini. Uwasilishaji na uchambuzi wa data umetumia mikabala ya kimaelezo na kiidadi. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kuna aina kuu tano za matatizo ya tafsiri katika ripoti za kitaaluma. Matatizo hayo ni tafsiri pana, tafsiri finyu, tafsiri potovu, matatizo ya kiisimu na matatizo ya kitahajia. Matatizo hayo yamesababishwa na wafasiri ambao wengi wao si mahiri wa LC na LL na hawana ujuzi kuhusu taaluma ya tafsiri. Wafasiri hawa pia hutumia visawe visivyofaa katika tafsiri, na kutokuwa makini katika uandishi na uhariri wa tafsiri. Hivyo, wafasiri wa ripoti za kitaaluma wanapaswa kuwa makini sana kwa sababu umuhimu wa tafsiri wanazozitoa mara nyingi huwa haulengi jumuiya moja mahususi bali aghalabu ni kwa binadamu wote. Utafiti huu umependekeza kwamba, kazi zote za tafsiri zifanywe na wataalamu wa tafsiri. Pia, wafasiri wawe na ujuzi wa lugha zote, yaani LC na LL. Vilevile, kiundwe chombo maalumu kwa ajili ya kusimamia na kutathmini ubora wa tafsiri kitaifa. Aidha, mtafiti anapendekeza kufanyika kwa utafiti kama huu kwa kuangalia nyaraka muhimu kama vile katiba ya nchi, katiba za vyama vya siasa na katiba za asasi zisizokuwa za serikali. Mwisho, badala ya kuangalia LL utafiti ufanyike kuangalia/kuchunguza matatizo ya LC katika tafsiri.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PE1498.2.S92S24)
Keywords
English language, Translating into Swahili, Swahili language
Citation
Saluhaya, M. (2014) Matatizo ya tafsiri katika ripoti za kitaaluma zinazofasiriwa kutoka kiingereza kwenda kiswahili, Master dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam