Matumizi ya vipengele vya kifani vya kingano katika mashairi ya kulikoyela kahigi: uchunguzi wa mashairi ya kisasa (1973) na mageuzi (2015)
dc.contributor.author | Ndumbaro, Eric Fortunatus | |
dc.date.accessioned | 2020-04-07T14:15:14Z | |
dc.date.available | 2020-04-07T14:15:14Z | |
dc.date.issued | 2017 | |
dc.description | Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.K33N3758) | en_US |
dc.description.abstract | Utafiti huu umechunguza matumizi ya vipengele vya kifani vya kingano katika mashairi ya Kulikoyela Kahigi ili kuona ufaafu wake katika jamii mamboleo na maendeleo ya ushairi andishi wa Kiswahili. Utafiti huu uliongozwa na malengo mahsusi matatu ambayo ni kubainisha vipengele vya kifani vya kingano kupitia mashairi ya Kahigi, kuchambua dhamira zinazoibuliwa kupitia vipengele vya kifani vya kingano pamoja na kujadili taathira za vipengele hivyo kwa ujumla. Data za utafiti huu zilikusanywa maktabani kutoka diwani za Mashairi ya Kisasa (1973) na Mageuzi (2015), pia kutoka katika maandiko mbalimbali. Data za uwandani zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya hojaji ambapo mwandishi wa diwani teule alipewa na kuijaza. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa kutumia nadharia ya mwingilianomatini iliyoasisiwa na Kristeva (1980). Nadharia ya mwingilianomatini humakinikia uchangamani na mwingiliano uliopo baina ya matini moja na nyingine. Sambamba na hayo, mkabala wa kitaamuli ulitumika katika kuwasilisha na kuchambua data za utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yamebaini kuwa vipengele vya kifani vya kingano kupitia mashairi ya Kahigi ni pamoja na; takriri, baalagha, muundo, mianzo na miisho ya kifomula, onomatopea, wahusika, mandhari, mtindo wa usimulizi kama vile monologia, dialogia, fantasia, taharuki na nyimbo. Vipengele hivi vimesaidia kuibua dhamira mbalimbali kama vile uzalendo, harakati za ukombozi Afrika, umuhimu wa utamaduni asilia, umuhimu wa uvumilivu katika maisha, matabaka katika jamii, uovu na uonevu katika jamii, ujasiri na mafanikio pamoja na mapinduzi. Vilevile, imebainika kwamba vipengele vya kifani vya kingano katika mashairi ya Kahigi huibua na kubeba taathira anuwai. Miongoni mwa taathira hizo ni pamoja na kuleta upya na kuboresha mtindo wa uandishi wa mashairi, kutajirisha mtindo wa uandishi wa mashairi, kuondoa ukavu katika mashairi, kusawiri tabia na matendo ya jamii, kuhifadhi utamaduni asilia na kupanua mawanda ya miundo ya mashairi. Vilevile hupanua mawanda ya uhakiki wa mashairi, hubainisha maudhui ya mashairi husika, huongeza idadi ya hadhira, hukanganya hadhira pamoja na kusaidia kukwepa udhibiti. Kwa ujumla, matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa matumizi ya vipengele vya kifani vya kingano yameleta upya katika ushairi andishi wa Kiswahili. Inapendekezwa kuwa watafiti wengine wanaweza kuchunguza matumizi ya fani nyingine za kijadi katika mashairi ya watunzi wengine wa mkondo wa kimapokeo au wa kisasa ili kuweza kubaini maendeleo yaliyofikiwa katika ushairi andishi. | en_US |
dc.identifier.citation | Ndumbaro, E.F. (2017) Matumizi ya vipengele vya kifani vya kingano katika mashairi ya kulikoyela kahigi: uchunguzi wa mashairi ya kisasa (1973) na mageuzi (2015). Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam. | en_US |
dc.identifier.uri | http://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/9153 | |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | University of Dar es Salaam | en_US |
dc.subject | Swahili poetry | en_US |
dc.subject | Kulikoyela kahigi | en_US |
dc.subject | Mashairi ya kisasa (1973) | en_US |
dc.subject | Mageuzi (2015) | en_US |
dc.title | Matumizi ya vipengele vya kifani vya kingano katika mashairi ya kulikoyela kahigi: uchunguzi wa mashairi ya kisasa (1973) na mageuzi (2015) | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |