Ufasihi wa maandishi ya sehemu za umma

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahusu ufasihi wa maandishi katika sehemu za umma, hususani vyooni Jijini Dar es salaam. Ingawa lengo ni kuangalia ikiwa kuna lugha ya kifasihi katika maandishi hayo. Aidha, kwa kutumia mbinu za utafiti makatabani kamavile uchambuzi matini na mbinu za uwandani kama vile ushuhudiaji, mtafiti alipata data muafaka kuhusu suala la kiutafiti liloshughulikiwa katika tasinia hii. Tasinifu hii imegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza, inahusu utangulizi wa jumla. Utangulizi huo umekusudia kubainisha na kupambanua upekee wa suala la dhima ya ubunifu unaojitokeza katika maandishi kwenye sehemu za umma, husussani katika kuta za vyoo. Ni katika utangulizi huo tumebainisha malengo , matilaba, mipaka na mawanda ya utafiti unaokusudiwa. Katika sura ya pili tumedurusu maandika mbalimbali yanayazungumzia au kuhakiki uandishi katika sehemu za umma na mitindo ya uandishi huo, na hasa namna lugha ilivyotumika kutoa mawasiliano. Aidha, ni katik sura hii tunazungumzia nadharia ya elimu mitindo amabyo ndiyo inayoongoza uchambuzi na mjada katika katika utafiti huu. Mbinu za utafiti zimefafanuliwa katika sura ya tatu. Miongoni mwa mbinu tunazojadli katika sura hii ni utafiti uliofanyika maktabani na mbinu za kukusanya data kutoka uwandani kama vile ushuhudiaji. Kimsingi, mbinu hizi zimesaidia kwa kiwango kikubwa ukusanyaji, uhifadhi na uchanganuzi wa data kama vile ilivyogdamiriwa. Katika sura ya nne tumewasilisha na kuchambua matokeo ya utafiti. Matokeo ya utafiti . Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa maandiko yaliyopo kwenye kuta za vyoo, yanajipambanua kiubunifu katika vipengele anuwai. Vipengele mardui vilivyojitokeza katika utafiti huu ni pamoja na matumizi ya lugha ya kisanaa iliyosheheni mbinu za kishairi, uchanganyaji wa lugha, misimu na misemo. Aidha kutokana na utafiti huu imebainika kuwa ubunifu huo unajitokeza pia katika kipengele cha maudhui, hususani dhamira. Dhamira zilizojitokeza zaidi ni zile zilizohusu maradhi, maarifa na dini. Ilibainika pia kuwa dhamira hizi zinaakisi muundo na mfumo wa jamii husika. Kutokana na matokeo haya, imethibitishwa kuwa ubunifu uliopo kwenye maandiko yaliyopo kwenye sehemu za umma unasawiri hali mbalimbali katika jamii jamii kama vile mtazamo wa wanajamii kuhusu maana na umuhimu wa elimu, dini, maadili na utamaduni kwa jumla. Sura ya mwisho katika utafiti huu ni ya kuhitimisha mjadala na kutoa mapendekezo. Katika sura hii, tumeeleza kwa kifupi yale ambayo tumeyajadili katika utafiti wote. Kutokana na matokeo ya utafiti huu inapendekezwa kuwa maandishi ya vyooni yachukuliwe kwa mtazamo chanya kama utanzu wa kifasihi unaoibuka. Umuhimu wa utafiti huu ni kujenga ari ya kiutafiti kuhusu fashi na kupanua wigo wa maana ya fasihi na tanzu zake.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr.Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL8703.M53)
Keywords
Graffiti, Swahili literature
Citation
Migodela, W (2011) Ufasihi wa maandishi ya sehemu za umma