Tofauti ya istilahi za Kisayansi kama zinavyotumiwa na TATAKI na BAKITA na athari zake kwa watumiaji wa lugha ya Kiswahili

Loading...
Thumbnail Image
Date
2016
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu ulikusudia kuchunguza tofauti ya istilahi za kisayansi kati ya BAKITA na TATAKI pamoja na athari zake kwa watumiaji wa lugha ya Kiswahili msisitizo ukiwa katika istilah za Kiswahili katika taaluma za Fizikia, Kemia na Bailojia. Data ya utafiti ilipatikana maktabani na uwandani. Utafiti wa Maktabani ulihusisha mapito mbalimabli kuhusu uundaji wa istilahi. Utafiti wa uwandani ulihusisha mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa data kama vile usaili, hojaji na majadiliano katika majopo. Kwa upande wa uchambuzi wa data mbinu ya kiidadi na kimaelezo zilitumika kuchambua data na kuwasilisha matokeo ya utafiti. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya jumla ya IstilahI (NJI) Iliyoasisiwa na Eugene Wuster 1931. Matokeo ya utafiti huu yalionesha kuwa kuna tofauti nyingi katika istilah za kisayansi kati ya BAKITA na TATAKI Kwa baadhiny dhana. Tofauti hizi zilibainishwa wazi kupitia machapisho mwili yaliyotumika kama mifano katika kuchunguza tofauti hizo. Sababu kubwa tuliyoigundua kama chanzo cha tofauti hizi ni kutokuwepo kwa ushirikiano miongoni mwa taasisi hizi wakati wa kuunda istilahi. Athari za tofauti zinazoletwa na tofauti za istilahi zilibainishwa amabzo ni pamoja na kutoueleweka kwa istilahi hizo miongoni mwa watumiaji wake hasa wataalamu wa uwanja uliotungiwa istilahi hizo pamoja na kupotosha matumizi ya lugha. Mapendekezo mbalimbalioya namna ya kukabili tatizo hili yametolewa ambapo ni pamoja na kushirikiana kwa taasisi zinazounda istilahi na kuwa na chombo kimoja kitachosimamia uundaji na usanifioshaji wa istilahi kwa kulindwa na kanuni za kisheria kwa lengo la kusimamia taasisi nyingine zinazounda istilahi. Aidha, katika utafiti huu yametolewa mapendekezo mbalimabli. Miongoni mwa mapendekezo ni kuchunguza vitabu vya sayansi katika shule za msingi ili kuona namna ambavyo waandishi wa vitabu hivi wanavyokabiliana na changamoto ya istilahi hizi.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr.Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL8703.N456)
Keywords
Swahili language, Terms and phrases, Science Issue Desk
Citation
Ngowi, R (2016) Tofauti ya istilahi za Kisayansi kama zinavyotumiwa na TATAKI na BAKITA na athari zake kwa watumiaji wa lugha ya Kiswahili, Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.