Mofosintaksia ya vitenzi vya kimashami kanuni za mwambatano wa ofimu nyambulisha kanuni za mwambatano wa mofimu nyambulishi

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu ulichunguza mofosintaksia ya vitenzi vya lugha ya kimashemi kwa malengo ya kubainisha kanuni za mwambatano wa mofimu nyambushi. Aidha, utafiti ulihusika kubaini namna ya utokeaji wa maumbo ya mofimu nyambulishi katika mzizi wa kitenzi. Utafiti ulidhihirisha kanuni zinazoruhusiwa na kanuni zuizi katika lugha kimashami.kazi hii inafungamanishwa na nadharia ya mofolojia Leksika (ML) ya Kiparsky (1982). Nadharia ya ML inadai kuwa uundaji wa maneno katika lugha hutegemea kanuni za mwambatano wa mofimu za lugha husika. Aidha, utafiti ulitumia kanuni tatu miongoni mwa kanuni kadhaa za nadharia ya ML ; kanuni za mzunguko kamili, kaida ya mfuto mabano na hifadhi miundo. data za utafiti huu ziliteuliwa kutoka kwa wazungumzaji wazawa, kamusi ya kimashami-kiswahili-kiingereza na vitabu mbalimbali vya kimashami. utafiti uligawanyika katika sura tano, sura ya kwanza, ilizungumziwa utangulizi wa jumla wa utafiti, sura ya pili, ilichambua na kuchanganua mapitio na maandishi yanayohusu sifa za mofimu nyambulishi katika lugha za kiulimwengu, kibantu na hatimaye kubainisha umuhimu wa utafiti katika lugha ya kimashami. sura ya tatu ilihusu mbinu zilizotumika zilizotumika katika ukusanyaji na uchambuzi wa data. katika sura ya nne, uchambuzi na usafiri wa data sanjari na utumizi wa nadharia ya ML vilianisha kanuni za mwambatano wa mofimu nyambulishi katika vitenzi vya kimashami. hatimaye sura ya tano, ilihitimisha na kutoa mapendekezo ya maoni yatakayotumika kama msingi na kichocheo cha tafiti za baadaye katika lugha ya kimashami na lugha nyengine za kiasili.
Description
Available in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL8110.C3L45)
Keywords
kimashani language, Chaga language, Morphemics, Kilimanjaro
Citation
Lema, Edda I (2011) Mofosintaksia ya vitenzi vya kimashami kanuni za mwambatano wa ofimu nyambulisha kanuni za mwambatano wa mofimu nyambulishi ,Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.