Tamthilia za kiswahili kuhusu ukimwi: ulinganishi wa upokezi kutoka kwa wanafunzi wa sekondari tanzania

No Thumbnail Available
Date
2011
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Slaam
Abstract
Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kubainisha na kulinganisha upokeaji wa tamthilia zinazohusu UKIMWI miongoni mwa wanafunzi wa sekondari katika Tanzania. Ili kukamilisha kazi hii, wanafunzi wa sekondari kutoka katika mkoa wa Dar es Salaam waliteuliwa kutoka katika shule tatu ambazo ni sekondari Tegeta, Benjamin Mkapa na Jitegemee. Aidha, Katika utafiti huu, tamthilia teule tatu zilitumika katika kufanya uchambuzi wa data ambazo ni Ngoswe Penzi Kitovu Cha Uzembe,Kilio Chetu na Orodha. Katika kukusanya na kuchambua data, marejeo mbalimbali yalitumika kutoka maktabani na uwandani. Pia mbinu mbalimbali zilitumika kukusanyia data. Zaidi ya hayo, uchambuzi wa data uliongozwa na nadharia ya Upokezi au Mwitiko wa msomaji kwa mujibu wa Stanley Fish (1980). Katika utafiti huu ingawa dhamira nyingi zinafanana, ilibainika kuwa wanafunzi wanapendelea zaidi tamthilia zinazoongelea UKIMWI kuliko zisizokuwa za UKIMWI. Jambo hili ni kinyume na matarajio ya kawaida, kwani katika tafiti nyingi (Taz. Dorothy Nelkin na wenzake, 1991) wasomaji hawapendelei kusoma kazi zinazohusu magonjwa au vifo. Upokezi wa tamthilia hizi miongoni mwa mbinu nyingine umehamasishwa na matumizi ya mbinu mbalimbali za lugha ya ubunifu ambayo imesheheni katika kazi hizi. Utafiti huu wa kiulinganishi utawasaidia wanafasihi hasa wale wa fasihi linganishi.Vilevile utafiti huu unapendendekeza kufanyika kwa kina tafiti katika tanzu nyingine za fasihi ili kuangalia upokezi na mwitiko wa jamii kwa ujumla kwa kuhususisha watu mbalimbali kama wazee na vijana ambao si wanafunzi.
Description
Available in print
Keywords
Swahili drama, Aids (Disease), Students, Secondary schools, Tanzania
Citation
Omary, M. (2011) Tamthilia za kiswahili kuhusu ukimwi: ulinganishi wa upokezi kutoka kwa wanafunzi wa sekondari tanzania. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Avaialble at http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx