Mvutano Kati Ya Maarifa Ya Kijaala Na Maarifa Ya Kijarabati Katika Maudhui Ya Filamu Za Kiswahili Nchini Tanzania

Loading...
Thumbnail Image
Date
2019
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es salaam
Abstract
Tasnifu hii inahusu mvutano kati ya maarifa ya kijjaala na maarifa ya kijarabati katika maudhui ya filamu za Kiswahili nchini Tanzania. Malengo mahususi yalikua manne ambayo ni kubainisha vipashio vya sanaa vinavyodokeza udhihirikaji wa maarifa ya kijaala na maarifa ya kijarabati, kuchambua dhamira zinazodokeza mvutano kati ya maarifa ya kijaala na maarifa ya kijarabati , kueleza sababu za kuzuka kwa mvutano katika jamii ya kitanzania. Data za maktabani zilikusanywa kwa kutazama sidii na data za uwandani zilikusanywa kwa mbinu ya hoja za usahili .Utafiti huu umetumia mkabala wa kitaamuli na mkabala wa kitakwimu.Mkabala wa kitaamuli ulisaidia kuchanganua data kutoka katika utazamaji wa filamu na data kutoka kwa watunzi wa filamu teule kwa njia ya usaili.Mkabala wa kitakwimu ulitumika kuchanganua data za hojaji toka kwa watazamaji ambazo ziliwekwa katika program ya SPSS. Data za uwandani zilikusanywa katika mikoa miwili, dar es salaam na Arusha. Idadi ya filamu teule n inane.mbili kwa kila mtunzi.Filamu hizo ni Gods kingdom na revelation za Emmanuel Myamba,Mkwe na Big surprise za Lea Mwendamseke, White Maria na point of no return za Mtitu Game na Jini Sonia na Radi Kobra za July Tax. Utafiti huu umeongozwa na nadharia mbili, semiotiki na Mwitiko wa msomaji.Nadharia ya semiotiki ilitumika katika lengo la kwanza na la pili. Utafiti huu uligundua kuwa , filamu teule zina vipashio9vilivyorejelewa pia kama misimbo na ishara) vingi vinavyodokeza dhana hizi mbili.Misimbo hiyo ni pamoja na wahusika , msimbo wa kiishara, msimbo wa kimatendo na matukio pamoja na mandhari.Aidha , utafiti huu umebaini kuwa , filamu teule zimejaa dhamira zenye mvutano kati ya ujaala na ujarabati ambazo ni pamoja na nguvu ya uhai, vifo na wafu,ukatili na utu, masuala ya kiuchumi, vyanzo vya magonjwa na matibabu yake,uchawi na uganga pamoja na mapenzi na ndoa . Watunzi na watazamaji pia walithibitisha kuwapo kwa maudhui yenye mvutano huu katika filamu nyingine za Kiswahili. Nadharia ya mwitiko wa msomaji, ilitumika katika lengo la tatu na lengo namba nne . Sababu za mvutano zilizopatikana kwa watunzi na watazamaji ni pamoja na uhalisia wa jamii ya kitanzania,tofauti za kimazingira na nyakati, changamoto za kiutafiti kwa watunzi,kutofautiana kwa viwango vya elimu, kujitosheleza kwa ujaala na ujarabati pamoja na mabadiliko katika tasnia ya filamu.Utafiti huu ulibaini kuwa , mvutano una athari chanya na hasi ambapo watafiti walitaja kuwa upotoshwaji wa jamii, kuijenga na kuielimisha jamii, kukuza migogoro, kupoteza imani kuchochea ugaidi pamoja na kudumaza uwezo wa kufikiri. Utafiti huu umesaidia kugundua vyanzo vya maarifa ya kisanaa kwa watunzi ambavyo ni vya kijaala na kijarabati vilevile.Aidha , ujaala ulionekana kutawala zaidi pamoja na kuwa sayansi na teknolojia inaaminika kutawala zaidi kwenye kila Nyanja ya maisha katika karne hii ya sasa. Utafiti umependekeza kuwapo kwa chombo kitakachohakiki kazi za watunzi kifalsafa .Chombo hicho kiwe na wataalamu wa ujenzi wa hoja na uchujaji wa hoja ili kulinda maarifa ya jamii na falsafa yake.Utafiti umebaini pia ufaafu wa nadharia ya semiotiki itumikapo pamoja na nadharia ya mwitiko wa msomaji katika kuchambua filamu nma vipengele vyake.Kutokana na ushikamani na ukamilishani wa nadharia hizi, utafiti huu umependekeza nadharia changamani kwa jina la semioiki-Mwitiko
Description
Available in print form,East Africana Collection ,Dr.Wilbert Chagula Library,Class mark (THS EAF PL8703.5T34C452)
Keywords
Swahili literature, Swahili drama, Content, Tanzania
Citation
Charles A (2019) Mvutano Kati Ya Maarifa Ya Kijaala Na Maarifa Ya Kijarabati Katika Maudhui Ya Filamu Za Kiswahili Nchini Tanzania,Master Dissertation,University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.