Mfungamano wa methali na shughuli za kiuchumi katika jamii ya wazigua

dc.contributor.authorMgallu, Amina
dc.date.accessioned2020-04-30T20:17:59Z
dc.date.available2020-04-30T20:17:59Z
dc.date.issued2012
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library,en_US
dc.description.abstractJapokuwa methali ni kipera kimojawapo kati ya vipera kadhaa vya fasihi simulizi kinachotumika katika maisha ya kila siku katika jamii, bado nafasi ya methali katika kuielewa mandhari na mazingira ya jamii inayotumia methali hizo haijatambuliwa na haijafanyiwa uchunguzi wa kina. Ili kubaini mfungamano wa methali na mazingira zinamotumiwa methali hizo, Tasinifu hii imejikita katika kutaflti juu ya mfungamano wa Methali na shughuli za kiuchumi katika jamii ya Wazigua. Methali zilizotumika katika utafiti huu zimetoka wilaya ya Handeni, mkoani Tanga. Malengo ya utafiti huu ni kutambulisha maana zinazopatikana katika methali za Kizigua, kubainisha shughuli za kiuchumi za Wazigua zinazojitokeza kupitia maana za methali hizo na kutathimini mfungamano uliopo baina ya shughuli hizo za kiuchumi na methali za jamii ya Wazigua. Kwa kutumia mbinu na nyenzo kadhaa katika kukusanya na kuchambua data kama vile kompyuta, kinasa sauti, kinyonyi, kalamu na shajara, malengo hayo yamefikiwa na kukidhi haja ya utafiti. Vilevile utafiti ulitumia mbinu za uwandani kama vile mahojiano na ushiriki, pia mbinu ya maktabani ambayo ni uchambuzi matini. Mbali na mbinu hizi mtafiti aliongozwa na nadharia ya Sosholojia kwa kuzingatia mwelekeo wa Rondon (1968) na kwa kutumia mkabala wa kitaamuli au mkabala wa maelezo katika kubaini mfungamano wa methali na shughuli za kiuchumi katika jamii ya Wazigua. Kutokana na utafiti huu, imebainika kuwa methali za Kizigua zinayasawiri mazingira ya jamii hii ya Kizigua.en_US
dc.identifier.citationMgallu, A (2012) Mfungamano wa methali na shughuli za kiuchumi katika jamii ya wazigua, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaamen_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/10593
dc.language.isoswen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaam,en_US
dc.subjectwaziguaen_US
dc.subjectLanguage acquisitionen_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.titleMfungamano wa methali na shughuli za kiuchumi katika jamii ya waziguaen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Amina Mgallu.pdf
Size:
9.28 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: