Usawiri wa mwanamke katika majigambo ya wahaya

Loading...
Thumbnail Image
Date
2016
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Tasinifu hii inachunguza na kuchambua Csawiri wa Mwanamke katika Majigambo ya Wahaya. Lengo kuu ni kubaini nafasi ya mwanamke katika jamii ya Wahaya. ili kutimiza lengo hilo, utafiti huu ulikuwa na malengo matatu mahususi ambayo ni : kubainisha usawiri wa mwanamke katika majigambo ya Wahaya, kueleza sababu za mwanamke kusawiriwa hivyo katika majigambo hayo na kueleza athazi za kifasihi na kijamii za usawiri huo wa mwanamke.Ili kutimiza malengo haya na kujibu maswali ya utafiti huu, mtafiti ametumia mbinu ya uwandani katika ukusanyaji wa data Katika kujibu maswali ya utafiti. Data ilikusanywa katika mkoa wa Kagera hasa katika wilaya ya Muleba katika kata za Nshamba, Biirabo, Kikuku na Muleba. Aidha, mtafiti ametumia mbinu ya maktabani katika kukusanya na kuwasilisha data kimaelezo. Uchambuzi na ufasiri wa data zilizokusanywa uliongozwa na nadharia ya ufeministi. Matokeo ya utafiti huu yanabainisha kuwa ijapokuwa majigambo ya Kihaya vapo ya aina mbalimbali, lakini yote yanamsawiri mwanamke katika namna chanya na hasi. Usawiri hasi ndio unaoonekana kuchukua nafasi kubwa. Sababu kuu ya mwanamke kusawiriwa hivyo katika majigambo ya Kihaya inabainika kuwa ni kutokana na masuala ya mila na desturi, dini, falsafa ya Kiafrika na utamaduni wa Kihaya kwa ujumla.
Description
Available in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library, class mark (THS EAF PL8237.4.K57)
Keywords
Haya language
Citation
Kitanga, F (2016) Usawiri wa mwanamke katika majigambo ya wahaya, Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.