Matumizi ya majina ya ukoo katika utambulisho wa jamii ya wasambaa

No Thumbnail Available
Date
2012
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahusu Matumizi ya Majina ya Ukoo katika Utambulisho wa Jamii ya Wasambaa. Utafiti huu ulilenga kubainisha maumbo ya majina ya ukoo yanayotambulisha jamii ya Wasambaa na kueleza asili na maana ya majina hayo ya ukoo. Utafiti huu uliongozwa na nadharia jumuishi ya Giles (1979) inayoelezea uhusiano wa lugha na utambulisho kwa kuzingatia fasili ya jamiilugha. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka wilaya ya Lushoto, kata za Mlalo, Malibwi na Vuga. Sampuli ya watafitiwa 60 ilihusishwa kwa njia ya usampulishaji nasibu tabakishi kwa kuzingatia kigezo cha umri. Mtafiti alitumia mbinu za hojaji na mahojiano katika ukusanyaji data. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kwamba majina ya ukoo 85 yanatumika kutambulisha jamii ya Wasambaa, kwa kiwango cha asilimia 60 mpaka 100 cha watafitiwa wote. Majina haya ni: Shetu(l)i, Shegao, Shenkondo, Shemalamba, Shemnkande, Shemnka(l)i, Shehoza, Kimweri, Maghisa, Mshakama(l)i, Mshilaghi, Shekinyashi, Shelubwaza, Shemandima, Shekizongolo, Shenkoba, Shemndolwa, Ngoma, Shezua, Shemakoko, Shemliwa, Sheshui, Shemaghembe, Shehemba, Sheka(l)aghe, Shekighenda, Kaniki, Kaoneka, Kwalazi, Mlindakumbi, Shekifumo, Gao, Gunda, Shekaholwe, Singano, Shekitundu, Shemayoya, Shemkiwa, Shemsanga, Mmaka, Chamshama, Shem'pemba, Shengoe, Chang'oa, Shechonge, Shehaghilo, Shechambo, Shekivuli, Shemweta, Kijazi, Shelukindo, Shemvua, Ngotonyingi, Mwambashi, Shemhilu, Shehiza, Sheshe, Shengoda, Shemkawa, Shemkiima, Shemghanga, Shemwaghulwa, Shembilu, Shewali, Shetumba, Shekidele, Shemkala, Shekimweri, Shembogha, Sheubua, Shemzighwa, Shemkong'wa, Shesighe, Shemtoi, Shemaua, Shunda, Shebughe, Shesaa, Shemandia, Shefovo, Sheghuio, Kanyawana, Mahim'phi, Shemdoe na Shedafa. Vilevile, matokeo ya utafiti yanadhihirisha kuwa majina mengi ya ukoo ya jamii ya Wasambaa yanatumia maumbo yanayoanza na kimbishi awali She + mzizi. Matokeo haya pia yamebainisha kuwa maana ya majina ya Kisambaa hutolewa kwa kuzingatia asili ya jina kwa kuzingatia matukio ya kijamii, tabia za watu, mabadiliko ya tabianchi, shughuli za kijamii na kiutawala, utani, mtu alikozaliwa na majina yatokanayo na majina ya wanyama na mimea. Ukubalifu wa majina haya una maana kwamba, jamii ya Wasambaa ina uelewa wa kutosha kuhusu majina ya ukoo na namna yanavyotambulisha jamii yao.
Description
Available in print form
Keywords
Sambaa language, Shambala language, Family names
Citation
Abel, E (2012), Matumizi ya majina ya ukoo katika utambulisho wa jamii ya wasambaa, master dissertation, University of Dar es Salaam (available at http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)