Utokeaji wa kiambishi tangulizi katika lugha ya kisubi

Loading...
Thumbnail Image
Date
2020
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es salaam
Abstract
Utafiti huu umechunguza utokeaji wa kimbishi tangulizi katika lugha ya Kiswahili. Lengo lilikuwa ni kuweka bayana maumbo na mazingira ya utokeaji wa kiambishi tangulizi katika lugha hiyo. Data ya utafiti huu ulikusanywa uwandani katika eneo la kata ya Nyaruhungo iliyopo wilayani Biharamuro, Mkoani Kagera. Mbinu ya hojaji na majadiliano ya vikundi lengwa zilitumika kukusanya data ya utafiti huu ulichambuliwa kwa mkabala wa kitaamuli ambapo mbinu ya uchambuzi wa data kimaudhui ilitumika.Nadharia ya Utangamano wa mfuatano wa mofimu ya McCalthy na princes (1995) imetumika katika uchanganuzi wa data. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa kiambishi tangulizi katika lugha tya kisubi kina maumbo sahili, yaani; maumbo ya irabu pekee. Maumbo hayo ni [a,e, i,o]. Aidha imebadilika kuwa maumbo hayo hutokea katika mazingira maluum ambayo ni bainifu. Mazingira hayo ni ya kategolia bainifu za maneno ya lugha hiyo zikiwa pwekepweke. Kulingana na utafiti huu kategolia hizo ni nomino, kivumishi, kielezi na kibainishi.Hata hivyo, kuna vighairi vichache vya kategolia hizo visivyokuwa na kiambishi tangulizi, hususan vivumishi viulizi na nomino zinazotaja majina ya ndugu kama vile maha (mama), kaaka (bibi) guuku (babu). Aidha ,imebainika kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika nomino iliopo kwenye kiima au kiarifu cha tungo hatakama tungo hiyo ina ukanushi , taarifa au masharti. Pia, utafiti huu umebaini kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika kielezi kinapoandamana na kitenzi katika tungo.Kadhalika,imebainika kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika nomino iliyopo kabla ya kibainishi kioneshi. Zaidi ya hayo, imebainilka kuwa kiambishi tangulizi hakitokei katika nomino iliyopo baadaya kibainishi kioneshi. Vilevile, utafiti huu umebaini kuwa kiambishi tangulizi hutokea kwenye kivumishi cha pekee kinachotanguliwa na nomino. Pia, imebainika kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika nomino iliyotanguliwa na kihusishi nomino ya uhusika milikishi na nomino iliotanguliwa na kiunganishi huru.Utokeaji huo hutokana na michakato udondoshaji, uunganishaji ua urefushaji wa irabu ya kihusishi, irabu ya kimilikishi au kiunganishi huru kilichotangulia nomino husika. Kwa hiyo, utafiti huu umebaini kuwa bazingira ya kimofolojia na kisintaksia ndiyo huamua kutokea au kutokutokea kwa kiambishi tangulizi katika lugha ya kisubi .Aidha utafiti huu umependekeza utafiti mwingine ufanyike katika kipengele cha ulinganishi wa ruwaza za utokeaji wa kiambishi tangulizi katika lugha mbalimbali za kibantu au zisizo za kibantu.
Description
Available in print form, Eat Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library,(THS EAF PL8025.T34J377)
Keywords
Bantu language, Kisubi, Tanzania
Citation
Jasson, T. (2020) Utokeaji wa kiambishi tangulizi katika lugha ya kisubi,tasnifu ya MA(kiswahili). Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Dar es Salaam.