Msamiati wa lahaja ya Kipemba unavyoweza kuchangia katika kiswahili sanifu

No Thumbnail Available
Date
2013
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu unaohusiana na mchango wa msamiati wa lahaja ya Kipemba kwa Kiswahili Sanifu ni kuchunguza msamiati wa lahaja hiyo na kuona mchango wake kwa Kiswahili Sanifu. Vipengele vilivyoshughulikiwa na utafiti huu ni pamoja na sauti za lahaja za Kipemba, sauti ambazo tumezifafanua kwa lengo la kubainisha mazingira ya ujitokezaji wa msamiati wa lahaja ya kipemba. Kipengele kingine kilichoshughulikiwa ni ubainishaji wa msamiati wa jumla na ule upatikanao katika uwanja (eneo) mahususi uhusuo shughuli za wakazi wa kisiwa cha Pemba kama vile uvuvi, ujenzi, mila na desturi na masuala ya ndoa, vyakula na vinginevyo mfano wa hivi. Kipengele cha mwisho kilichoshughulikiwa ni ufafanuzi wa msamiati wa lahaja ya Kipemba ambao unaweza kuchangia katika Kisanifu. Utafiti huu umetumia mkabala wa Isimufafanuzi unaohusu uchunguzi na ufafanuzi wa vipengele vya lugha vilivyo(vinavyosemwa) au vilivyokua vikisemwa kwa wakati fulani. Mkabala huu umeweza kuuongoza utafiti huu kwa kufafanua msamiati wa lahaja ya Kipemba na mchango wake kwa Kiswahili Sanifu. Matokeo yameonyesha kwamba msamiati wa lahaja ya Kipemba una mchango mkubwa katika kuwakilisha dhana kadhaa za kiutamaduni na dhana nyingi ambazo hazijapata uwakilishi katika Kiswahili Sanifu.
Description
Kinapatikana Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya East Africana, (THS EAF PL8704.Z9M63)
Keywords
Kiswahili language, Pemba Island (Tanzania)
Citation
Mohammed, S. H (2013) Msamiati wa lahaja ya Kipemba unavyoweza kuchangia katika kiswahili sanifu, Tasnifu ya M.A. (Kiswahili), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam