Uhusiano wa Dhamira na Mandhari katika Riwaya ya Ziraili na Zirani ya W.E. Mkufya
Loading...
Date
2012
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam,
Abstract
Utafiti huu ulichunguza Uhusiano wa Dhamira na Mandhari katika Riwaya ya Ziraili na Zirani. Sura ya kwanza ni utangulizi wa jumla wa tasinifu. Tatizo lililojenga utafiti huu ni kutokana na hali ya mazoea ya kuhakiki kazi za fasihi na kuelezea dhamira peke yake na mandhari peke yake kama vipengele viwili vinavyotofautiana. Hivyo utafiti huu ulijikita katika kuchunguza jinsi dhamira zinavyohusiana na mandhari katika riwaya ya Ziraili na Zirani. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani na uwandani katika kupata data muhimu zilizokamilisha tasinifu nzima. Ruwaza ya jumla ilipatikana kuhusu mwingiliano na usababishano wa vipengele vya fani na maudhui baada ya uchambuzi wa kina wa vipengele hivyo. Utafiti uliongozwa na nadharia ya usababishi ili kuonesha uhusiano uliopo kati ya dhamira na mandhari. Na hivyo ilibainika kwamba matukio yatokeapo huibua mahali, wakati na mazingira. Hivyo matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba kuna uhusiano mkubwa unaotokana na sababu za kisababishi, yaani kila kimoja kinasababisha kingine kutokea. Utafiti huu umependekeza uchambuzi zaidi wa kitaaluma ufanyike hasa katika riwaya ya Ziraili na Zirani, jam bo ambalo litasaidia kurahisisha usomekaji na uchambuzi hasa kwa wasomaji wachanga wa kazi za kifasihi. Pia utafiti huu umependekeza kuwa, wanazuoni wanapaswa kuchunguza usababishano wa fani na maudhui na uhusiano wa vipengele vyake, na sio kuchambua kila kimoja peke yake kwani kila kimoja kinaweza kusababisha chenzake kutokea.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.K52)
Keywords
Swahili literature, Ziraili na ziarni, Mkufya W.E
Citation
Kibakaya, R (2012)Uhusiano wa Dhamira na Mandhari katika Riwaya ya Ziraili na Zirani ya W.E. Mkufya, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam