Maana na misingi ya uteuzi wa majina ya watu katika lugha ya kiha
No Thumbnail Available
Date
2014
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Unversity of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umechunguza Maana na Misingi ya Uteuzi wa Majina ya watu katika lugha ya Kiha. Utafiti ulilenga kubainisha na kujua maana, dhima na sababu zinazochochea utoaji wa majina ya watu. Utafiti umefanyika katika kata za Muhinda na Mwayaya, wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma, Tanzania. Ili kufanikisha kazi hii, Nadharia ya Ufungamanishi ya Hallowell (1955) ilitumika kuongoza utafiti huu. Nadharia hii hueleza kwamba kuna mfungamano kati ya wanadamu na mazingira ambapo binadamu hudumisha na kuendelea kujitambua kwa njia ya kujikumbusha uzoefu wa nyuma. Utafiti ulihusisha sampuli ya watafitiwa 90 ambapo usampulishaji nasibu tabakishi ulitumika kwa kutumia kigezo cha umri. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu za hojaji, mahojiano na hifadhi ya maandishi na kisha kuchanganuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa majina ya watu katika jamii ya Waha hudokeza maana mbalimbali kama vile tabia, matukio, mahusiano, uzazi au ugumba, matatizo, kushukuru na kueleza nyakati au majira. Vilevile ni nyenzo muhimu ya kutunza kumbukumbu na kueleza historia na uchumi wa jamii. Vilevile utafiti umebaini sababu mbalimbali zinazochochea utoaji wa majina ya watu katika jamii ya Waha kuwa ni mila na desturi, sifa au tabia za mtoto au mtu, imani kwa wahenga na mizimu, imani kwa Mungu, maumbile na muonekano, masaibu mbalimbali, hali ya ujauzito na matatizo ya uzazi yaliyotangulia, mfuatano katika kuzaliwa, muda na kipindi ambacho mtoto alizaliwa, pamoja na kuendeleza ukoo. Hivyo majina ya watu hutumika kama njia ya ya kueleza utamaduni, maisha, mahusiano na kutunza kumbukumbu za jamii husika. Kulingana na umuhimu huo, kuna haja ya kufanya tafiti juu ya lugha na mazingira kwani vijana wengi wameathiriwa na utandawazi, huku suala la utamaduni wao likiachwa. Ingefaa kutumia hazina ndogo ya wazee iliyobaki ili kuhifadhi tamaduni zetu hususani jamii ya Waha
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8025.T34J66)
Keywords
Kiha language, Kiha (African people), Names, Personal, Language, Bantu language, Tanzania