Tofauti za kiisimu baina ya kiswahili cha micheweni na kiswahili cha wete katika kisiwa cha Pemba

No Thumbnail Available
Date
2011
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza tofauti za kiisimu baina ya Kiswahili cha Micheweni na Kiswahili cha Wete katika kisiwa cha Pemba. Utafiti unaendeleza mbele hatua za kuitafiti lugha ya Kiswahili na lahaja zake ambapo kazi hii inatoa mawazo ya awali katika kuelezea tofauti za kiisimu za Viswahili vizungumzwavyo katika maeneo hayo. Data ya uwandani ya utafiti huu umekusanywa kwa kutumia mbinu za usaili, hojaji na ushuhudiaji ambapo sampuli-tegemea fursa na sampuli eneo zimetumika kuchagua watoa taarifa kwa vigezo vya umri na ukazi. Vifaa kama vile tepu rekoda, kompyuta, kalamu, karatasi na jalada vimetumika wakati wa kukusanya, kuchambua na kuwasilisha data. Nadharia ya isimulinganishi na mbinu za uchambuzi matini zimetumika kuchambua data hiyo. Katika vipengele vya fonolojia, msamiati, mofolojia na miundo ambavyo vimechunguzwa, Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa kuna tofauti kubwa za kiisimu baina ya Kiswahili cha Micheweni na Wete. Hivyo, Kiswahili cha Micheweni kinaonekana kuhifadhi msamiati na miundo mingi ya Kiswahili cha kale (lahaja) ambapo Kiswahili cha Wete kwa kiasi kikubwa kinaelekea kwenye usanifu. Kwa vile, utafiti huu unabainisha kuwa kuna tofauti kubwa za kiisimu baina ya Kiswahili cha Micheweni na Kiswahili cha Wete, utafiti huu hauhitaji hitimisho la haraka. Uchunguzi zaidi unahitaji kuchunguza chanzo na sababu za tofauti hizo.
Description
available in print
Keywords
Swahili language, Phonology, Micheweni district, Wete district, Pemba Island
Citation
Juma, H.K (2011) Tofauti za kiisimu baina ya kiswahili cha micheweni na kiswahili cha wete katika kisiwa cha Pemba, master dissertation, University of Dar es Salaam, (availalbe at http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)