Muundo wa kirai kitenzi katika lugha ya kisambaa

dc.contributor.authorHabibu, Nasra
dc.date.accessioned2019-06-22T07:30:05Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:36Z
dc.date.available2019-06-22T07:30:05Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:36Z
dc.date.issued2011
dc.descriptionAvailable in printen_US
dc.description.abstractUtafiti huu, unachunguza muundo wa Kirai Kitenzi katika lugha ya Kisambaa. Mtafiti anachunguza ni vipashio gani vinaandamana na vitenzi katika sentensi za Kisambaa. Uchunguzi huu wa Kirai Kitenzi cha Kisambaa umefanyika kwa kutumia nadharia ya Sarufi Jumuishi ya Miundo Virai. Nadharia hii ni mojawapo ya nadharia za Sarufi Miundo Virai, zinazotumika kuelezea sintaksia ya lugha. Ni nadharia iliyoanzishwa na Gerald Gazdar mwaka 1970. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa kitenzi cha Kisambaa kinaweza kisifuatiwe na kipashio chochote au kinaweza kuandamana na vipashio mbalimbali kama vile Kirai Nomino, Kitenzi kisaidizi, sentensi, Kirai Kielezi na Kirai Kihusishi. Hivyo Kirai Kitenzi cha Kisambaa kinaundwa na Kitenzi kimoja; Kitenzi na Kirai Nomino chenye nomino moja au mbili; Vitenzi viwili; Kitenzi na Kiunganishi tegemezi na Sentensi; Kitenzi, Kirai Nomino, Kiunganishi tegemezi na Sentensi; Kitenzi na Kirai Kihusishi; Kitenzi na Kirai Kielezi. Pamoja na hayo vilevile katika utafiti huu imebainika kuwa dhana ya uelekezi wa vitenzi inajitokeza pia katika vitenzi vya Kisambaa. Hii ni kwa sababu kuna Virai Vitenzi vinavyoundwa na kitenzi pamoja na Kirai Nomino chenye nomino moja ama mbili, pia vitenzi ambavyo si lazima viandamane na nomino bali vipashio vingine kama kielezi.en_US
dc.identifier.citationHabibu, N. (2011) Muundo wa kirai kitenzi katika lugha ya kisambaa. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Available athttp://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspxen_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3398
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectShambala languageen_US
dc.titleMuundo wa kirai kitenzi katika lugha ya kisambaaen_US
dc.typeThesisen_US
Files