Dhima ya nyimbo za msiba katika jamii ya wahehe
No Thumbnail Available
Date
2013
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Makusudi makuu ya utafiti huu yalikuwa ni kuchunguza ili kubaini dhima ya nyimbo za msiba katika jamii ya Wahehe. Pamoja na lengo hili, mtafiti aliweka malengo mengine madogo ambayo ni kubaini matukio na shughuli zinazoibua nyimbo katika jamii ya Wahehe, na pia kuzibainisha nyimbo hizo za jamii ya Wahehe. Utafiti huu ulianzia maktabani kwa kusoma maandiko mbalimbali yahusuyo nyimbo kwa jumla na nyimbo za jamii ya Wahehe kwa upekee, jambo lililosaidia katika kubaini tatizo la utafiti, ambalo lilimpeleka mtafiti uwandani katika Mkoa wa Iringa, wilaya ya Iringa, tarafa ya Mlolo, kata ya Luhota, katika vijiji vya Tagamenda na Kitayawa, ambako mtafiti alikusanya data zinazohusu nyimbo za msiba za jamii ya Wahehe. Data zilikusanywa kwa watafitiwa walioteuliwa, hususani wasanii wa nyimbo za msiba. Vifaa mbalimbali kama vile simu, kalamu, daftari, kamera, na kompyuta vilitumiwa na mtafiti alipokuwa uwandani. Vifaa hivi vilitumiwa pamoja na mbinu zilizotumiwa na watafiti kama vile, usaili, ushuhudiaji pamoja na majadiliano ya vikundi. Baadaye data zilichakatwa na kuchambuliwa kwa kuongozwa na nadharia ya usosholojia. Data zilizochambuliwa zilitoa majibu ya maswali ya utafiti, hususani kubainisha matukio yanayoibua nyimbo ambayo ni biashara, kilimo na harusi. Kubainisha nyimbo za msiba za jamii ya Wahehe. Kueleza dhima ya nyimbo za msiba katika jamii ya Wahehe, kama vile kuliwaza wafiwa, kutambulisha msiba, na pia kukumbusha matukio mbalimbali katika jamii ya Wahehe na jamii kwa ujumla. Mapendezo kuhusu tafiti zijazo yametolewa mwishoni.
Description
Available in print copy
Keywords
Hehe language
Citation
Kapinga, A.(2013). Dhima ya nyimbo za msiba katika jamii ya wahehe. Master dissertation, university of Dar es Salaam. Available at (http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)