Usawiri wa mwanamke katika tamthilia ya Kiswahili ya kimfumojike mifano kutoka mama mtakatifu (1982) na kivuli kinaishi (1990)

Loading...
Thumbnail Image
Date
2019
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umechunguza uwasiri wa mhusika mwanamke katika tamthilia ya Kiswahili ya kimfumojike ukijikita katika tamthilia ya Mama Mtakatifu (1982) na Kivuli Kinaishi (1990) ili kubaini ujitokezaji wa mwanamke anayesawiri mfumojike katika tamthilia. Utafiti huu uliongozwa na malengo mahususi matatu ambayo ni, mosi, kufafanua sifa za muhusika mwanamke anaye wasiri mfumojike katika tamthilia hizo teule, pili kubainisha dhamira zitokanazo na sifa za mhusika mwanamke anayewasiri mfumojike katika tamthilia hizo teule, na tatu, kuchambua dhima ya ujitokezaji wa mhusika mwanamke anayewasiri mfumojike katika tamthilia hizo teule kwa maendeleo ya fasihi. Data za utafiti huu zilikusanywa maktabani. Uchambuzi wa data ullifanywa na kutumia nadharia ya Ufemanisti wa Kiafrika. Nadharia ya ufemanisti wa kiafrika humakinikia uhusiano wa yale yanayoandikwa katika fasihi na mtazamo wake juu ya mwanamake wa kiafrika na dispora. Sambamba, na hayo mkabala wa kitaamuli ulitumika kuwasilisha na kuchambua data za utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yamebaini utokezaji wa mhusika mwanamke anayewasiri mfumojike katika tamthilia tajwa. Sifa zake ni mwanamke ndiye kiongozi wa juu, mweye mamlaka ya kuamua bila kuhojiwa, msimamizi wa shughuli za sherehe za kitamaduni na huongoza akisaidiana na baraza la wazee. Aidha, husimamia afya za wanajamii, ndiye kiongozi wa majeshi na mtetezi wa jamii, mrithi, muundaji na msimamaiaje wa utekelezaji wa sheria. Mbali ya sifa hizo pia mwananamke hufanya maamuzi kushirikisha na wengine, mwenye umri mkubwa na mwisho huwa na nguvu za sihiri na uganga. Sifa hizi zinaibua dhamira zifuatazo , uongozi, ushawishi na werevu, busara na utu katika maamuzi, afya kwa wanajamii, utawala wa sheria, uwajibikjai na uzalendo, ujasiri na uganga na sihiri. Fauka ya hayo, imebainika kwamba uwasiri huo wa mhusika mwanamke ana dhima kadha wa kadha katika maendeleo ya fasihi nazo ni kuibua mkondo wa tamthilia ya Kiswahili usiozoeleka, pili, kuibua mkondo usiozoeleka na uwasiri wa mwanamke katika fasihi ya Kiswahili. Tatu, kuendeleza nadharia ya Ufemanisti wa Kiafrika, nne kuendeleza ontolojia ya Kiafrika, tano, kutanganisha fasihi andishi na fasihi simulizi. Kwa ujumla, matokeo ya utafiti huu yanaonsha susawiriwa kwa mhusika mwanake anayesawiri mfumojike katika tamthilia ya Kiswahili. Inapendekezwa kua watafiti wengine wachunguze usawiri wa mhusika mwanamke wa kimfumojike katika tamthilia za watunzi wa fasihi wanawake na pia katikat tanzu zingine. Kwa wahakiki wa watunzi wa fasihi ya Kiswahili inapendekezwa washughulikie masuala ya kijamii hususani tamaduni zinazoonekana kutopewa umuhimu katika kuchunguzwa na kuandikiwa kama utamaduni wa mfumojike katika fasihi ya Kiswahili.
Description
Available in print form, Eat Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library,(THS EAF PL8704.D5227)
Keywords
Swahili drama, Mama Mtakatifu(1982), Kivuli Kinaishi (1990)
Citation
Didas, L. K. (2019) Usawiri wa mwanamke katika tamthilia ya Kiswahili ya kimfumojike mifano kutoka mama mtakatifu (1982) na kivuli kinaishi (1990). tasnifu ya MA(kiswahili). Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Dar es Salaam.