Ukanushi wa vishazi katika kiswahili sanifu

No Thumbnail Available
Date
2015
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Suala la ukanushi limejadiliwa na wataalamu mbalimbali. Pamoja na hivyo, hakuna utafiti uliofanywa kuhusu ukanushi wa vishazi katika Kiswahili sanifu. Utafiti huu ulikuwa na lengo la kuchunguza ukanushaji wa vishazi huru na tegemezi katika Kiswahili sanifu. Sura ya kwanza inahusu malengo ya utafiti huu ambayo ni kubainisha vipashio vya ukanushi wa vishazi huru na vishazi tegemezi kwa kuwa wataalamu wametaja baadhi. Lengo la pili ni ubainishaji wa nafasi ya vipashio vya ukanushi katika vishazi huru na vishazi tegemezi na chanzo cha tofauti zake kwa kuwa suala hili halijaelezwa na wataalamu. Lengo la tatu ni kubainisha utokeaji wa mofimu ya njeo na nafsi yake. Utafiti huu utawanufaisha wanaisimu, wazungumzaji na wanaojifunza Kiswahili sanifu. Sura ya pili inahusu mapitio na machapisho mbalimbali yanayohusu mada ya utafiti. Pia ilihusu nadharia ya Minimalisti ambayo ilitumika kufanya uchambuzi wa data za utafiti huu. Sura ya tatu ilishughulikia mbinu za utafiti na ukusanyaji wa data, nazo ni mbinu za uwandani, dodoso pamoja na hojaji katika ukusanyaji wa data. Sura hii pia inaangazia mbinu ya uchanganuzi wa data ambapo mbinu ya kimaelezo ilitumika. Sura ya nne inahusu uwasilishaji na uchanganuzi wa matokeo ya utafiti. Sura ya tano inahusu matokeo ya utafiti nayo ni kuwepo kwa tofauti katika ukanushaji. Pia sura ina hitimisho na mapendekezo kwa ajili ya uboreshaji wa uchunguzi na isimu kwa ujumla.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8702.K38)
Keywords
Swahili language, Grammar
Citation
Kawale, F. R. (2015) Ukanushi wa vishazi katika kiswahili sanifu, Master dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam