Namna vitendawili vya wanyakyusa vitokanavyo na mabadiliko ya kijamii
No Thumbnail Available
Date
2012
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Tasinifu hii ilichunguza namna vitendawili vya Wanyakyusa vitokanavyo na mabadiliko ya kijamii. Ili kutimiza azma hiyo, tasinifu hii ilifanyika uwandani kwa kutumia mbinu ya hojaji na dodoso. Pia, iliongozwa na nadharia ya Uhistoria Mpya. Kanuni ya msingi katika nadharia hii ni kuitalii fasihi na kuikita katika muktadha wa kihistoria na kuuelewa utamaduni na historia yake kupitia kazi za kifasihi. Utafiti ulibaini kuwa upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya vitendawili na mabadiliko yatokeayo katika jamii hasa ukichunguza maudhui yake pamoja na lugha iliyotumika. Kwa jumla, tasinifu hii imeonesha kuwa mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi, mwingiliano wa jamii na maendeleo ya sayansi na teknolojia ni nyenzo muhimu katika kusanifu maudhui na lugha ya vitendawili vinavyohakiki mabadiliko hayo. Tasinifu hii imependekeza kuwa, kutokana na tanzu za fasihi simulizi na vipera vyake kuwa na tabia ya kuingiliana, kuna haja ya kufanya utafiti jumuishi utakaohusisha vipera vingine vya semi katika jamii ya Wanyakyusa kama vile, methali, nahau, misemo na mafumbo. Mwisho, tasinifu hii imedokeza maeneo mengine ambayo yanatakiwa kufanyiwa utafiti zaidi katika baadhi ya vipengele vya kifani kama vile, muundo, mtindo, wahusika na mandhari ambavyo havijachunguzwa kutokana na mipaka ya utafiti aliyojiwekea mtafiti.
Description
Available in print form
Keywords
Nyakyusa language, Nyakyusa
Citation
Mwangosi, G (2012) Namna vitendawili vya wanyakyusa vitokanavyo na mabadiliko ya kijamii, Master dissertation, University of Dar es Salaam. (Available at http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/search.aspx?)