Usawiri wa wanawake katika fasihi ya Kiswahili: ulinganifu wa waandishi wa kike na wa kiume – uchunguzi katika riwaya teule

No Thumbnail Available
Date
2011
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Tasnifu hii inachambua jinsi wahusika wakuu wanawake walivyosawiriwa katika riwaya za Kiswahili zilizoandikwa na waandishi wa kike na wa kiume. Kwa kufanya hivi, tasnifu inafanya ulinganishi wa waandishi wa riwaya teule za: Rosa Mistika (Kezilahabi, 1971), Nyota ya Rehema (Mohamed, 1976), Shida (Balisidya, 1981) na Hiba ya Wivu (Mwanga, 1984). Lengo kuu ni kuona ikiwa kuna tofauti baina ya waandishi wa kike na wa kiume katika kumchora mhusika mkuu mwanamke. Maswali kadhaa yanaibuliwa ikiwa ni pamoja na ni kwa kiasi gani mwandishi ni mtu huru anayeweza kuihakiki kwa uyakinifu jamii iliyomlea na kumkuza? Je mwandishi anajitenga kiasi gani na mila na desturi ambazo yeye mwenyewe anazipiga vita? Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ile ya Ufeministi, ambayo inaangalia uhusiano uliopo kati ya mwanamume na mwanamke. Kwa hakika tunazingatia tawi moja la nadharia hii, lile la Ufeministi wa Kiafrika ambalo ni nadharia inayoshughulikia matatizo ya wanawake na namna ya kuyatatua matatizo ya mwanamke wa kiafrika. Mbinu za utafiti zilizotumika ni pamoja na kusoma, kudurusu vitabu, majarida na nyaraka mbalimbali katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili kuweza kupata data. Katika uchambuzi imeonekana kuwa hakuna tofauti ya msingi baina ya waandishi wa kike na wale wa kiume. Wote wamemchora mwanamke katika taswira hasi. Jambo hili linatuonesha kuwa waandishi hawaandiki kiholela holela tu kwa kuwa wao ni wanaume au wanawake, bali huandika wakianini kwamba, wao ni chombo cha kijamii na ni sehemu ya jamii wanayoiandikia. Jamii hizi ni zile zilizozungukwa na mila, desturi na zaidi mambo haya yanakuzwa na mhimili na mawazo yanayoshadidiwa na dini. Utafiti huu unapendekeza elimu iwe mkombozi kwa mwanamke ili ajikomboe kutokana na mfumo wa ukandamizaji. Elimu hii itasaidia wanajamii kuondokana na mawazo potofu ya kusema kuwa nafasi aliyopewa mwanamke ni mapenzi ya Mungu na ndiyo stahili yake.
Description
available in print form
Keywords
Swahili literature
Citation
Lyatuu, J (2011)Usawiri wa wanawake katika fasihi ya Kiswahili: ulinganifu wa waandishi wa kike na wa kiume – uchunguzi katika riwaya teule, master dissertation, University of Dar es Salaam(available at http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)