Dhamira kwenye nyimbo za wasanii wasioona na mtazamo wao kwa jamii

No Thumbnail Available
Date
2011
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahakiki na kubainisha dhamira mardudi zinazojitokeza kwenye nyimbo za waimbaji wasioona na kujadili mtazamo wao kwa jamii inayowazunguka kuhusu hali zao. Dhamira zinahakikiwa kwa kuzingatia masuala ya kijamii, kiuchimi, kisiasa na kiutamaduni. Dhamira zinahusishwa na mtazamo wao kwa kuangalia kinachosemwa na waimbaji wasioona kuhusu wao wenyewe na hali zao, ushiriki wao katika shughuli za kijamii, matatizo wanayokutana nayo na wengine katika jamii. Kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa mashairi, (Wamitila, 2008), ambayo inachunguza utanzu wa ushairi na uhusiano uliopo baina ya ushairi na muktadha, mtafiti alikusanya mashairi yaliyoimbwa na waimbaji wasiona na kupata data iliyofanyiwa uchambuzi. Data hiyo hatimaye ilifanyiwa uchambuzi kwa kutumia nadharia ya kisosholojia, ambayo inashikilia kuwa uhusiano kati ya fasihi na jamii ni muhimu sana. Katika uchambuzi imeonekana kuwa waimbaji wasioona wanatumia nyimbo zao kudai haki na usawa kwa walemavu wote. Mtazamo wao ni kuwa jamii inawatenga na kuwaona hawana thamani katika jamii. Msimamo wao ni kuwa wao wana uwezo wa kusoma, kufanya kazi na kushiriki katika shughuli zote za kijamii, wanachohitaji ni ushirikiano na kusaidiwa pale wanaposhindwa. Utafiti umebaini kuwa waimbaji wasioona huzungumzia pia masuala ya watu wengine katika jamii ambayo ni kero, kama ugonjwa wa UKIMWI, mapenzi na ndoa na nafasi ya mwanamke na mwanaume katika jamii.
Description
Available in print form
Keywords
Swahili literature, Poetry, Blind musicians
Citation
Chamba, L.A (2011)Dhamira kwenye nyimbo za wasanii wasioona na mtazamo wao kwa jamii, master dissertation, University of Dar es Salaam(available at http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)