Ufungamano wa tamathali za semi na maudhui : Uchunguzi wa nyimbo za Unyago wa mwanahiti wa Wazaramo

Loading...
Thumbnail Image
Date
2016
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unaohusu ufungamano wa Tamathali za Semi na Maudhui: uchunguzi wa nyimbo za unyago wa mwanahiti wa Wazaramo ulisukuma na ukweli kuwa suala l a ufungamano wa fani na maudhui katika nyimbo za unyago, halijashughulikiwa vya kutosha. Hivyo, utafiti huu ulikusudia kueleza unyago wa Wazaramo na nafasi ya nyimbo za unyago wa Mwanahiti wa Wazaramo na; kujadili mfungamano wa tamathali za semi zilizojitokeza na maudhui. Ili kutimiza malengo hayo, utafiti huu ambao data yake ilikusanywa katikaa mkoa wa Pwani na Dar es salaam ulitumia mbinu ya mahojiano, ushiriki, ukusanyaji matini na utafiti wa maktabani. Pia, utafiti huu uliongozwa na nadharia ya usosholoji na nadharia ya umuundo na mkabala wa kitaamuli katika kuchambua na kutafsiri data zilizokusanywa. Matokeo ya utafiti yamebainisha kwamba unyago katika jamii ya Wazaramo, ni asasi muhimu snaya kurithisha amali mbalimabli. Pia, imebainka kuwa kuna aina mbalimabali za unyago katika jamii ya Wazaramo amabzo zinatumia nyimbo zilizosheheni tamathali za semi. Si hivyo tu bali pia imebainika kuwa kuna mfungamano mkubwa baina ya tamathali za semi zilizotumika na maudhui yanayowasilishwa na nyimbo za unyago wa Mwanahiti. Tamathali mbalimali za semi zinanaonekana kuisaidia kuibua dhamira, kutambulisha wahusika, kubeba falsafa na dhima nyingine kadhaa wa kadha za kifani na kimaudhui. Ingawa utafiti huu umejadili kwa kina masuala mbalimabli yanayohusiana na ufungamano wa fani na maudhui katika unyago wa Wazaramo, bado panahitajika tafiti za kina kushughulikiaa ufungamano huo katiak tanzu nyinginezo za fasihi ili kuweza kutoa mahitimishi jumuishi. Pia, kwa utafiti huu ulihusu aina moja ya unyago wa Wazaramo, unyago wa Mwanahiti, kuna haja ya kufanya utafiti katiak aina nyingine za unyago wa jamii hii na hata jamii nyinginezo. Aidha, kuna haja ya kufanya utafiti wa ufungamano wa vipengele vingine vya fani katika kuwasilisha maudhui.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr.WilbertChagula Library, (THS EAF PL8702M39)
Keywords
Swahili language, Zaramo (African people), Figures of Speech
Citation
Mayemba, T (2016) Ufungamano wa tamathali za semi na maudhui : Uchunguzi wa nyimbo za Unyago wa mwanahiti wa Wazaramo, Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.