Mbinu za utunzi wa nyimbo ndefu: uchunguxi wa nyimbo katika ngoma ya wagashe
Loading...
Date
2012
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam,
Abstract
Utafiti huu ulichunguza Mbinu za Utunzi wa Nyimbo Ndefu za Ngoma ya Wigashe, ya jamii ya Wasukuma. Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuzibaini Nyimbo Ndefu na Mbinu za Utunzi wa Nyimbo hizo. Data zilipatikana katika wilaya ya Kwimba kwa kuwahoji manju na wafuasi, kusikiliza nyimbo na kuzirekodi na zilitumika kama data za msingi. Matokeo yameonesha kuwa, nyimbo ndefu za Wigashe zinajulikana kwa jina la Migololo, Maliliko, Mihilili au Busoloja. Maneno hayo ya Kisukuma yanatambulisha urefu wa kitu. Urefu wa nyimbo hizi hupimwa kwa kutumia vigezo mbalimbali. Kigezo kimojawapo ni muda unaotumika katika uimbaji wa wimbo mmoja mfululizo ambazo ni dakika 25 hadi 180. Kigezo kingine ni kutumia idadi ya vijiti ambapo katika uimbaji, urefu wa nyimbo hutegemea uchache au wingi wa vijiti vilivyohesabiwa wakati wa mashindano. Tatu ni nyimbo ndefu kuwekwa kama sharti la msingi wakati wa kumpata mshindi katika mashindano ya ngoma ya Wigashe. Mbinu zilizobainika ni pamoja na uwezo wa manju wa kufafanua mambo mengi yaani (Jitulo) katika wimbo mmoja Mbinu nyingine ni urudiaji wa maneno, udokezi nyuma na mbele na uchepukaji wa mada Utafiti umebaini pia kuwa kuna mbinu ya utendaji wa kisanaa, yaani mbwembwe na manjonjo ya wachezaji na upigaji wa ala za muziki hurefusha muda, yaani wakaa. Mbinu ya kurefusha muda hutumika mwanzo, kati au mwishoni mwa wimbo. Licha ya kufanikiwa kwa malengo ya utafiti, bado kuna haja ya kufanyika tafiti nyingine katika uwanja huu, hususan kuonesha uhusiano kati ya fasihi simulizi na mambo mbalimbali yaliyomo katika jamii za kiafrika zikiwamo nyimbo
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8694.S94B82)
Keywords
Sukuma language, songs, Traditional Dances, Wigashe Dance, Sukuma (African People)
Citation
Budebah, Chr B (2012),Mbinu za utunzi wa nyimbo ndefu: uchunguxi wa nyimbo katika ngoma ya wagashe, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam