Fonolojia ya kiswahili cha mwambe
No Thumbnail Available
Date
2012
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unaohusu fonolojia ya Kiswahili cha Mwambe unajaribu kuelezea na kujadili mifumo ya sauti za Kimwambe pamoja na michakato ya kifonolojia na athari zake katika irabu na konsonanti. Kazi hii imegawika katika sura nne. Sura ya kwanza ni utangulizi ambao unazungumzia usuli, mahali pa utafiti, tatizo, malengo, maswali, umuhimu na mipaka ya utafiti. Vipengele vingine vilivyozungumziwa katika sura hii ni pamoja na mapitio ya maandiko, mbinu za ukusanyaji na uchambuzi wa data, nadharia iliyoongoza utafiti na uwasilishaji wa data. Sura ya pili inahusu mifumo ya sauti za Kimwambe zinavyotofautiana au kufanana na Kiswahili sanifu. Tumefafanua irabu, konsonanti na viyeyusho. Pia, tumejadili miundo ya silabi za Kimwambe. Miundo inayobainishwa katika sura hii ni : Muundo wa silabi unaohusu irabu pekee, nazali pekee, konsonati na irabu, konsonanti mbili na irabu, konsonanti kiyeyusho na irabu na kiyeyusho na Irabu. Sura ya tatu inaelezea na kujadili michakato ya kifonolojia inayoathiri irabu na konsonanti. Michakato inayohusu irabu ni udondoshaji wa irabu, muungano wa irabu, tangamano la irabu, uyeyushaji, urefushaji wa irabu, unazalishaji wa irabu, na uchopekaji wa irabu. Aidha, sura hii inabainisha mchakato mmoja unaoathiri konsonanti ambao ni utamkiaji pamwe wa nazali. Sura ya nne inatoa kwa ujumla muhutasari wa mjadala, matokeo ya utafiti na inajibu maswali ya utafiti. Kadhalika sura hii inatoa hitimisho, maoni na mapendekezo vii kuhusu maeneo yanayohitaji kufanyiwa utafiti zaidi.
Description
Available in print form
Keywords
Swahili language, Phonology, Pemba Island, Tanzania
Citation
Juma, S.U.(2012). Fonolojia ya kiswahili cha mwambe. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Available at (http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx?parentpriref=)