Usawiri wa mhusika mwanamke katika tamthilia ya kilio cha haki na nguzo mama

No Thumbnail Available
Date
2012
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unakusudia kuangalia Usawiri wa Mhusika Mwanamke katika Tamthilia ya Kilio cha Haki na Nguzo Mama. Malengo ya utafiti huu ni kuonyesha na kubainisha namna mwandishi mwanamke na mwanaume wanavyomsawiri mhusika mwanamke katika tamthilia teule, na kueleza jinsi usawiri wa mhusika mwanamke unavyojenga dhamira katika tamthilia ya Kilio cha Haki (1981) na Nguzo Mama (1982). Katika utafiti huu mbinu ya maktabani imetumika. Mtafiti ameweza kusoma, kudurusu vitabu, majarida na nyaraka mbalimbali katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili kupata data ya kazi yake. Matokeo ya utafiti huu yameonyesha kwamba, mwandishi mwanamke na mwanaume wote kwa pamoja wameweza kumsawiri mhusika mwanamke katika tamthilia ya Kilio cha Haki na Nguzo Mama kwa upande chanya na upande hasi. Pamoja na hivyo, tumegundua mwandishi mwanamke amehusika zaidi katika kumdhalilisha mhusika mwanamke. Kwa upande mwingine, mwandishi mwanaume amejaribu kumpamba mhusika mwanamke kwa kumpa sifa chanya, japokuwa mwisho wa kitabu anaamua kumporomosha mhusika huyo. Hivyo basi, ni vizuri waandishi hawa wote kwa pamoja, wakaandika kazi zao kwa kueleza usawiri wa wahusika wao, kwa kuwafanya kama vielelezo katika jamii badala ya kuendelea kuwadunisha. Utafiti huu unapendekeza tafiti zaidi kuhusiana na tanzu zingine za fasihi ili kuweza kupima matokeo ya utafiti kama yatakuwa ni yaleyale au tofauti.
Description
Available in print form, East Africana collection, Dr. Wilbert Chagula Library, class mark (THS EAF PL8704.K35)
Keywords
Swahili drama, Kilio cha haki, Nguzo mama
Citation
Kamba, T.P (2012) Usawiri wa mhusika mwanamke katika tamthilia ya kilio cha haki na nguzo mama, Tasinifu ya M.A Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)