Browsing by Author "Peterson, Rhoda"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Matumizi na dhima za lugha katika mandhari-lugha ya jiji la Dar es salaam(University of Dar es Salaam, 2014) Peterson, RhodaShauku ya kuchunguza eneo la mandhari-lugha inaendelea kukua miongoni mwa watafiti wa lugha kutokana na kushamiri kwa maandishi katika sehemu za wazi. Ulinganishaji wa maandishi binafsi na ya kiserikali umekuwa kama msingi wa tafiti za kimandhari-lugha. Kigezo hiki pekee hakiakisi matumizi halisi ya lugha katika eneo hilo kwani linahusisha shughuli tofauti za kijamii. Utafiti huu wa matumizi na dhima za lugha katika mandhari-lugha ya jiji la Dar es Salaam umefanywa kwa kuzingatia muktadha wa kibiashara. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya semiotiki-jamii ya Halliday inayochunguza lugha kwa kuihusisha na jamii. Data zilizoko kwenye mfumo wa kongoo-andishi zilikusanywa kwa njia ya kupiga picha. Ushuhudiaji wa huduma zitolewazo madukani na mahojiano kwa wafanyabiashara zilikuwa njia za nyongeza za ukusanyaji wa data. Ufafanuzi wa data ulifanywa kwa kutumia njia ya uchambuzi mada. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa Dar es Salaam ni jiji lenye matumizi ya wingilugha. Lugha zilizobainika kutumiwa ni Kiingereza, Kiswahili, lugha za asili, Kiarabu, Kichina, Kihindi, na Kikorea. Lugha ya Kiingereza inatawala kimatumizi ikifuatiwa na Kiswahili, kisha lugha zingine zimetumiwa kwa kiasi kidogo sana. Dhima za lugha zilizodhihirika ni kukaribisha na kushawishi wateja wanunue bidhaa, kutambulisha bidhaa, jamii mbalimbali na imani za kidini. Kutokana na data za utafiti huu inapendekezwa kwamba muktadha wa matumizi ni kipengele kingine kinachoweza kutumiwa kuchunguza matumizi ya lugha katika mandhari-lugha. Vilevile, maudhui ni kipengele kinachoweza kutumiwa kuchunguza dhima za lugha katika mandhari-lugha.Item Policy makers` views on the language medium of instruction in Tanzania secondary and tertiary education(University of Dar es Salaam., 2008) Peterson, RhodaPlans were made in Tanzania in the 1980s on the possibilities of extending Kiswahili as the language medium of instructions (henceforth LOI) to post- primary education. Since then, there have been significant research reports and publications on the question of LOI in Tanzania. Most of these research endeavors show that English is an obstacle to the teaching and learning processes at post-primary levels. Yet the LOI issue has not yet been resolved. This study examines the views of policy makers who seem to let the situation continue as it in spite of the research outcomes and classroom practices that English can not longer serve as an effective LOI in post primary levels. It is revealed in this study that Kiswahili can cater for secondary as well as tertiary levels. Since 69.8% of them are in favor of English and who do not believe in the research findings. Conversely, the discussion reveals that any society can sustainability develop and industrialize if a familiar language to its members is being used as the LOI in education. Additionally, it is argued in the present work that proficiency in English is not attained through using it as a medium instruction. The use of the familiar language as the medium instruction facilitates not only students to understand the subject matter. Hence the dissertation indicates that the use of Kiswahili at the LOI in Tanzania will not only strengthen the teaching and learning process, but also it will facilitate the acquisition of English and often foreign language skills when such languages are taught efficiently and effectively as subjects.