Browsing by Author "Mwendamseke, Faraja Japhet"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Mkazo Katika Kiswahili Sanifu(University of Dar es Salaam, 2019) Mwendamseke, Faraja JaphetUtafiti huu ni wa kifonolojia uliochunguza mkazo katiak Kiswahili sanifu. Jumla ya watoa taarifa 20 wamehusika katika kutoa data iliyotumika katika utafiti huu. Watoa taarifa 10 walitoka kata ya Ngamiani Kati na Chumbageni katiak jiji la Tanga, mkoani Tanga. Watoa taarifa wengine 10 walitoka katiak Jiji la Tanga, mkoani Tanga. Watoa taarifa wengine 10 walitoka katika shehia ya Mkunazini na Shehia ya Malindi, UNGUJA MJINI, Zanzibar. Taarifa hizo zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano na ushuhudiaji. Utafiti huu ni wa kiidadi na kimaelezo ambao umefanyika kwa kuongozwa na nadharia ya Fonolojia Mizani. Data zilizokusanywa zilichunguzwa kwa kusikilizwa kwa makini na kwa kutumia program ya “Praat”. Aidha, matokeo ya utafiti huu yaonesha kuwa uchunguzi wa mkazo katika kiwango cha neon hujibainisha tofauti na mkazo katika kirai na sentensi. Mara nyingi mkazo msingi katiak neon hutokea katika silabi ya mwisho kasa moja, wakati mwingine mkazo msingi hutokea katiak katika silabi ya mwisho katika vihisishii. Kwa upande wa kirai na sentensi mkazo msingi hutokea katika neno la mwisho katiak tungo husika. Hata hivyo, katiak Kiswahili sanifu imebainika kuwa licha ya kuwepo mkazo msingi katika neno, kirai na sentensikuna aina nyingine pia za mkazo. Yaani mkazo upili, mkao utatu na mkazo dhaifu, kutegemeana na namna utamkaji unavyojidhihirisha katika neno, kirai na sentensi kuna aina nyingine pia za mkazo. Yaani mkazo wa pili, mkazo utatu na mkazo dhaifu, kutegemeana na namna utamkaji unavyojidhirisha katika viambajengo hivyo. Kwa hiyo, kila kiambajengo kinakiasi Fulani cha nguvumsikiko. Pia, licha ya ruwaza ya mkazo kuwa funge kama ilivyoelezwa na wataalamu wengine kama vile Halle naClements (1983) na Massamba (2011). Utafiti huu umeenda mbele zaidi na kubaini kuwa ruwaza ya mkazo inaweza kuathiriwa na michakato ya kifonolojia kama vile udondoshaji, michako ya kimofolojia kama vile uambatani na uradidi. Aidha, katika uamilifu wa mkazo utafiti huu umebaini kuwa na uaminifu ufuatao: kwanza ni kuwekewa nguvu katika silabi au neno wakati wa utamkaji ili kuonesha msigano wa msikiko katika viambajengo vinavyohusika. Pili, kuna wakati mkazo huwa na uamilifu wa kuonesha msisitizo katika kiambajengo kinachohusika yaani katika neno, kirai au sentensi. Tatu mara chache mkazo huweza kubadili maana ya msingi ya msingi ya neno, hutokea katika baadhi ya maneno mkazo unapohama. Aidha, kutokana na uamilifu wa mkazo tumeweza kutofautisha mkazo na kiimbo pamoja na kidatu katika katika Kiswahili sanifu. Hata hivyo, kuna mazingira mengine kiimbo na kidatu huweza kuathiri mkazo lakini athari hiyo ya kimsikiko haibadili uamilifu wa mkazo.Item Uanishaji wa ngeli za nomino katika lugha ya Ki-bena.(University of Dar es Salaam, 2011) Mwendamseke, Faraja JaphetUtafiti huu unahusu uainishaji wa ngeli za nomino za lahaja ya Ki-Mwasamu ya lugha ya Ki-bena inayozungumzwa kusini magharibi mwa Tanzania katika wilaya ya njombe mkoani Iringa. Jumla ya watafitiwa 29 kutoka kata ya Imalinyi, lgima na Mdandu ndio waliohusika. uteuzi wao ulikuwa wa kinasibu. Taarifa zimekusanywa kwa watafitiwa kwa njia ya hojaji, mahojiano na ushuhudiaji. Utafiti huu ulikuwa na malengo yafuatayo: kubainisha ngeli za Ki-Bena na idadi yake, kuchunguza mtawanyiko wa nomino zenye asili moja kisemantiki katika ngeli zilizoundwa kwa msingi wa kimofolojia na kufafanua dhima mbalimbali zinazojitokeza katika viambishi ngeli vya nomino. lli kutimiza malengo haya mikabala mitatu ya kinadharia imetumika ambayo ni: mkabala wa Viambishi Awali vya Nomino, mkabala wa Viambishi vya Upatanisho wa Kisarufi na mkabala wa Kisemantiki. Mkabala wa Viambishi Awali vya Nomino umetumika kubainisha viambishi ngeli vya nomino katika misingi ya umoja na wings. Aidha mkabala wa Viambishi vya Upatanisho wa Kisarutl umetuinika pia kutokana na nomlno zmgine kutokuwa na viambishi dhahiri vya urnojzt na wingi. Katika uchunguzi wetu tumebaini kuna ngeli za Ki-Bona 18. Mkabala wa Kisemantiki umetumika kuchunguza mtawanyiko wa nomino zenye asili moja kisemantiki katika ngeli za msingi wa kimofolojia. Imebainika mtawanyiko wa nomino katika lugha ya Ki-bena upo katika nomino za viungo vya mwili, matunda, na wanyama. Mtawanyiko kama huu haupo katika nomino zinazohusu binadamu. Hivyo inatofautiana sana na lugha kami vile Kiswahili. Pia utafiti huu umebaini katika- lugha ya Ki-Bena, viambishi ngeli vya nomino vina dhima kama vile umoja/wingi, ukubwa/udogo na uzuri/ubaya. Dhima zote hizi huweza kujitokeza katika kiambishi kwa wakati mmoja na kusababisha utata. Pia kuna upekee unaojitokcza katika dhitna ya uzuri na ubaya ambapo dhima ya ubaya hutumika kwa binadamu na viumbe wanaufungwa na binadamu tu, lakini dhima ya uzuri ni kwa wote.