Browsing by Author "Kawale, Fatuma Ramadhani"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Ukanushi wa vishazi katika kiswahili sanifu(University of Dar es Salaam, 2015) Kawale, Fatuma RamadhaniSuala la ukanushi limejadiliwa na wataalamu mbalimbali. Pamoja na hivyo, hakuna utafiti uliofanywa kuhusu ukanushi wa vishazi katika Kiswahili sanifu. Utafiti huu ulikuwa na lengo la kuchunguza ukanushaji wa vishazi huru na tegemezi katika Kiswahili sanifu. Sura ya kwanza inahusu malengo ya utafiti huu ambayo ni kubainisha vipashio vya ukanushi wa vishazi huru na vishazi tegemezi kwa kuwa wataalamu wametaja baadhi. Lengo la pili ni ubainishaji wa nafasi ya vipashio vya ukanushi katika vishazi huru na vishazi tegemezi na chanzo cha tofauti zake kwa kuwa suala hili halijaelezwa na wataalamu. Lengo la tatu ni kubainisha utokeaji wa mofimu ya njeo na nafsi yake. Utafiti huu utawanufaisha wanaisimu, wazungumzaji na wanaojifunza Kiswahili sanifu. Sura ya pili inahusu mapitio na machapisho mbalimbali yanayohusu mada ya utafiti. Pia ilihusu nadharia ya Minimalisti ambayo ilitumika kufanya uchambuzi wa data za utafiti huu. Sura ya tatu ilishughulikia mbinu za utafiti na ukusanyaji wa data, nazo ni mbinu za uwandani, dodoso pamoja na hojaji katika ukusanyaji wa data. Sura hii pia inaangazia mbinu ya uchanganuzi wa data ambapo mbinu ya kimaelezo ilitumika. Sura ya nne inahusu uwasilishaji na uchanganuzi wa matokeo ya utafiti. Sura ya tano inahusu matokeo ya utafiti nayo ni kuwepo kwa tofauti katika ukanushaji. Pia sura ina hitimisho na mapendekezo kwa ajili ya uboreshaji wa uchunguzi na isimu kwa ujumla.