Browsing by Author "Daniel, Zawadi Limbe"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Mkabala wa Kibwege katika fasihi ya Kiswahili Mifano Kutoka Tamthilia ya Amezidi (1995) Said A. Mohamed(University of Dar es Salaam, 2012) Daniel, Zawadi LimbeFasihi ya Kiswahili imepita katika mikabala mbalimbali, mkabala wa Kibwege1 ni mojawapo ya ikabala hiyo. Mkabala huu unaelezwa kuibuka baada ya vita vya pili vya dunia huko Ulaya ambapo, inadaiwa kuwa kuibuka kwake kulitokana na kukata tamaa kwa watu baada ya ugumu wa maisha ulijotokeza mara baada ya kumalizika kwa vita hivyo. Wilson na Alvin (1991) Mkabala huu unatajwa na baadhi ya wahakiki kujitokeza katika tamthilia ya Kiswahili hususan ile ya mwandishi Said A. Mohamed. Huyu ni mwandishi aliyebobea katika utunzi wa kazi za fasihi, hususan tamthilia, riwaya, hadithi fupi na ushairi. Baadhi ya tamthilia zake ni Pungwa (1988), Kivuli Kinaishi (1990), Amezidi (1995), Kitumbua Kimeingia Mchanga (2000), na Posa za Bi Kisiwa (2007). Amezidi (1995) ni moja kati ya tamthilia zenye mtindo wa kipekee katika fasihi ya Kiswahili. Wahakiki wa kazi za fasihi ya Kiswahili kama vile Wamitila (2003), na Njogu na Chimerah (2008) wameitaja tamthilia hii kuwa ni miongoni mwa tamthilia za Kiswahili za mkabala wa Kibwege. Tasnifu hii imechambua na kubainisha sifa na vipengele vya fasihi ya Kibwege na namna vinavyojitokeza katika tamthilia hii ya Amezidi. Aidha, inaeleza namna muktadha wa Tanzania baada ya uhuru ulivyochangia kuibuka kwa thieta ya Kibwege katika fasihi ya Kiswahili. Katika tasnifu hii muktadha unaojadiliwa ni ule wa kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisanaa. Vilevile, nafasi na mchango wa matumizi ya mkabala huu katika fasihi ya Kiswahili vyote vinajadiliwa katika tasnifu hii.Item Ujitokezaji wa tashtiti katika fasihi ya Kiswahili: Uchunguzi wa kazi teule(University of Dar es Salaam, 2019) Daniel, Zawadi LimbeUtafiti huu ulichunguza ujitokezaji wa tashtiti katika kazi za fasihi ya Kiswahili ukiongozwa na malengo mahsusi matatu ambayo ni kubainisha mbinu zinazotumika kuunda tashtiti, kueleza dhima ya tashtiti na kuainisha tashtiti katika kazi za fasihi ya Kiswahili. Uchunguzi wa ujitokezaji huu ulifanywa kupitia kazi teule za fasihi ya Kiswahili za: Kaptula la Marx 9Kezilahabi, 1999), Amezidi (Mohamed, 1995), Walenisi (Mkangi, 1995), na Miradi Bubu ya Wazalendo (Ruhumbika, 1992). Utafiti huu ulitumia mbinu ya uchambuzi matini na mkabala wa kitaamuli. Aidha nadharia za semiotiki-jamii na Mwingiliano- matini ziliongoza utafiti huu. Matokeo katika utafiti huu yanaonesha tashtiti katika kzi teule ni mtindo wa kisanaa unaoundwa kwa kutumia mbinu za dhihaka, kejeli, ufyosi, matumizi ya tamadhali ya usemi hasa sitiari, tashbiha na uchuku ubeuzi, taswira na ishara, mandhari pamoja na ujenzi wa wahusika. Matokeo haya yanapingana na madai yaliyokwishatolewa na Msokile (1992), Mbonde (2002), Senkoro(2011), na Wamitila (2003) kwamba tashtiti katika fasihi ya Kiswahili hujitokeza kama kipengele cha kitamathali pekee, madai ambayo yalichukulia tashtiti kuwa kipengele kinachofungamanishwa na matumizi ya lugha pekee. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa tashtiti ni dhana pana, ambayo katika kujipambanua kwake inatumia si tu vipengele vya lugha na kitamathali, bali pia mbinu mbalimbali za kifani na kimaudhui. Vilevile, matokeo yanaonesha kuwa tashtiti ina dhima kuu tatu katika kazi teule za fasihi ya Kiswahili. Dhima hizi ni za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Katika dhima ya kisiasa tashtiti inahakiki uongozi, inakemea rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, inapinga ukoloni mamboleo na utegemezi wa misaada, na inatathimini utoaji wa haki na usawa. Katika dhima ya kiuchumi tashtiti inaumbua hali ya umaskini, na inashambulia hali ya utabaka. Kijamii tashtiti ina dhima ya kukosoa mfumo wa elimu, kuhakiki utamaduni na maadili na pia kuumbua hali duni za afya na uzazi . Aidha utafiti huu umependekeza aina tano za tashtiti ambazo ni tashtiti ya mtindo jumuishi, tashtiti –tamathali, tashtiti-husika, tashtiti-ufyosi na tashtiti-fiche. Kutokana na matokeo ya utafiti huu uainishaji huu ndiyo unafaa kumika katiak kazi za fasihi ya Kiswahil