Browsing by Author "Chitimbe, Barnaba"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Usawiri wa mwanamke katika nyimbo za ngoma ya mganda ya Wanyasa.(University of Dar es Salaam, 2014) Chitimbe, BarnabaUtafiti huu uliazimia kutimiza lengo kuu ambalo lilikuwa ni kubainisha jinsi dhamira za nyimbo za ngoma ya Mganda ya Wanyasa zinavyomsawiri mwanamke. Katika utafiti huu nadharia za ufeministi na uhalisia zilitumika sambamba na mbinu ya ushuhudiaji na mahojiano katika kukusanya data. Aidha uchambuzi wa data uliongozwa na mkabala wa kitaamuli kwa kiasi kikubwa na takwimu zilitumika pale tu zilipohitajika.Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba nyimbo za ngoma ya Mganda ya Wanyasa zimemsawiri mwanamke katika mtazamo hasi na chanya. Katika mtazamo chanya mwanamke ameelezwa kuwa na thamani kubwa kutokana na kuwa mchapakazi hodari, mshauri mzuri katika jamii, mvumilivu na kama mama na mlezi mzuri wa watoto. Katika mtazamo hasi, mwanamke ameelezwa kuwa ni kiumbe anayenyanyasika na kugandamizwa katika jamii kwani jamii inamchukulia mwanamke kuwa ni mtu asiye na haki mbele ya mwanamume, mtu mwenye wivu, mshirikina, malaya, mtu wa kukaa nyumbani na ni kiumbe tegemezi kwa mwanamume. Mwisho hitimisho la utafiti limedhihirisha kwamba jamii inapaswa kuelimishwa ili kuacha kumkandamiza mwanamke pamoja na kuondoa mtazamo hasi dhidi ya mwanamke.