Mwambapa, Elisha2021-02-082021-02-082016Mwambapa, E. (2016) Ulinganishiwa Kiisimu katika Lahaja za kingondena ki-mwamba za lugha ya Kinyakyusa, Master dissertation, University of Dar es Salaamhttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/14671Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8549.M8521)Utafiti huu ulikuwa ni mchakato wa kuchunguza mfanano na tofauti za kiisimu baina ya lahaja ya Ki-Ngondena Ki-Mwamba ilikuthibitisha kama Ki-Ngondena Ki-Mwamba ni lahaja za lugha moja, ni lugha mbili tofauti au sio lahaja bali ni lugha moja tu. Utafiti huu umefanyika katika vijiji vya Ndalana Lugombo katika wilaya ya Rungwe na vijiji vya Ngeleka na Makwale katika wilaya ya Kyela katika mkoa wa Mbeya. Mbinu za utafiti zilihusu usampulishaji na sampuli, na mbinu za ukusanyaji data na mbinu za uchambuzi wa data. Data ya utafiti iliyohusika katika utafiti huu ni data ya kutoka uwandani ambapo maswali mbalimbali yaliulizwa ilikujazwa na watoa taarifa. Msamiati wa lugha ya Kiswahili uliteuliwa ili watoa taarifa waingize tafsiri ya lugha ya Kinyakyusa kwa kufuata lahaja wanazozitumia. Utafiti huu ulitumia pia data ya Kinyakyusa kwa kufuata lahaja wanazo zitumia. Utafiti huu ulitumia pia data ya maktabani, (upitia maandiko. Kazi hii imegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza inaeleza juu ya kiini cha tatizo na mbinu ambazo zimetumika katika kufikia mahitimisho. Sura ya pili imeshughulikia mapito mbalimbali ya maandiko yanayohusu lahaja katika lugha za kibantu ambazo zimewahi kuandikiwa. Sura ya tatu imejihusisha na kujaadili mbinu mbalimbali za utafiti ambazo ni sampuli na usampulishaji mbinu za kukusanya data ni mbinu zilizotumika kuchanganua data. Suraya nne imeshughulikia uwasilishaji na uchanganuzi wa data. Data za uwandani zimechanganuliwa kwa njia yamaelezo na majedwali. Uchanganuzi huu wa data umeongezwa na. Nadharia ya Isimu Linganishi na Nadharia Tete ya Ndugu wa karibu na Ndugu wa Mbali ya Nadharia ya makutano na Mwachano. Sura ya tano imeshulikia matokeo ya utafiti, hitimisho na mapendekezo ya tafiti fuatishi. Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa Ki-Ngondena Ki-Mwamba ni lahaja zinazokaribiana sana zenye tofauti ndogondogo sana. Kutokana na matokeo hayo tunahitimisha kuwa Ki-Ngondena Ki-Mwamba n ilahaja za lugha ya Kinyakyusa zenye tofauti ndogondogo.swNgondo languageMwamba languageNyakyusa languageUlinganishiwa Kiisimu katika Lahaja za kingondena ki-mwamba za lugha ya KinyakyusaThesis