Sovu, Yahya Ahmad2021-10-082021-10-082020Sovu, Yahya Ahmad (2020) Uchanganuzi wa mbinu za kisarufi na kibalagha katika vilongo teule vya kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015, nchini Tanzania,PhD Thesis , University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.http://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/15925Available in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL 8704.T34S598)Utafiti huu ulilenga kuchunguza lugha ya kisiasa, hususani katika kipindi cha kampeni za uchaguzi wa 2015 nchini Tanzania. Hoja kuu ikiwa ni kuchambua kwa undani mbinu za wanasiasa na nduni anuwai wanazozitumia katika mikutano ya kampeni za uchaguzi. Ili kutimiza hoja hii utafiti ulilenga hasa kubaini nduni za kisarufi na kibalagha katika vilongo teule vya hotuba za kampeni za uchaguzi za mwaka 2015, kuchunguza dhima zake katika kampeni za uchaguzi na kupambanua iwapo mbinu hizo zina athari chanya na hasi kwa hadhira. Data za utafiti zilikusanywa maktabani na uwandani kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa nyaraka, usikilizaji wa hotuba, usomaji wa maandiko, usaili, na hojaji. Mkabala wa kitaamuli, na wa kiidadi kwa kiasi kidogo ilitumika kuchambua data zote. Mkabala wa Uchanganuzi Tunduizi Kilongo pamoja na Nadharia ya Balagha zimetumika katika utafiti huu. Matokeo ya utafiti yameonesha kwamba, hali ya ukinzani baina ya kambi za UKAWA na CCM imejidhihirisha katika lugha za kampeni kupitia mbinu za uteuzi wa maneno, vijenzi vya sarufi na tamathali za kibalagha. Matokeo yameonesha zaidi kuwa, kauli zenye kutweza afya ya wagombea, kejeli, kashfa na vitisho zilitumiwa. Pia, kauli zenye kuhimiza amani, mshikamano, kufanya kazi kwa bidii zilisikika. Matumizi ya nafsi ya kwanza "ni-", lugha za mitaani, takriri, jazanda, chuku, misimu, methali, mbazi za kidini, sitiari na vionjo anuwai vya lugha vilifumbatwa iii kufikia malengo hayo. Vilevile, matokeo yameonesha kwamba, mbinu hizi zina dhima ya urembeshaji, ufafanuaji, usisimuaji, uthibitishaji na hata ujikurubishaji kwa hadhira. Pia, imebainika kwamba, mbinu za kisarufi na kibalagha zimeibua athari chanya za kuburudisha, kuhimiza, kuzindua, kujenga matumaini na athari hasi zinazochochea ubaguzi, udhalilishaji, na kujenga uhasama miongoni mwa wanajamii.Utafiti huu umechangia katika taaluma ya uchanganuzi vilongo. Mchango mahususi umejikita katika kubaini sifa za lugha ya kampeni za kisiasa kama rejista maalumu. utafiti huu unapendekeza wazungumzaji katika hotuba za kampeni za uchaguzi wazingatie matumizi mazuri ya lugha yenye kujenga umoja na mshikamno, pia waache kuendeleza matumizi ya lugha zisizo za staha, matusi na kejeli ambazo zinaweza kuchochea migogoro miongoni mwa hadhira wanazozihutubia.swSwahili languageGrammarcomperation and generalElectionTanzaniaUchanganuzi wa mbinu za kisarufi na kibalagha katika vilongo teule vya kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015, nchini TanzaniaThesis