Jasson, Tasiana2021-10-152021-10-152020Jasson, T (2020). Utokeaji wa kiambishi tangulizi katika lugha ya kisubi. Tasinifu ya uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Dar es Salaamhttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/16076Available in print form, EAF Collections, Dr. Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL8025.T34J377)Utafiti huu umechunguza utokeaji wa kiambishi tangulizi katika lugha ya Kisubi Lengo lilikuwa kuweka bayana maumbo na mazingira ya utokeaji wa kiambishi tangulizi katika lugha hiyo. Data ya utafiti huu ilikusanywa uwandani katika eneo la Kata ya Nyarubungo iliyopo Wilayani Biharamulo, Mkoani Kagera. Mbinu ya hojaji na majadiliano ya vikundi lengwa zilitumika kukusanya data ya utafiti huu. Aidha, data ya utafiti huu ilichambuliwa kwa mkabala wa kitaamuli ambapo mbinu ya uchambuzi wa data kimaudhui ilitumika. Nadharia ya Utangamano wa Mfuatano wa Mofimu ya McCarthy na Prince (1995) imetumika katika uchanganuzi wa data. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa kiambishitangulizi katika lugha ya Kisubi kina maumbo sahili, yaani; maumbo ya irabu pekee. Maumbo hayo ni [a, e, i, o]. aidha, imebainika kuwa maumbo hayo hutokea katika mazingira maalumu ambayo ni bainifu. Mazingira hayo ni ya kategoria hizo ni nomino, kivumishi, kielezi na kibainishi. Hata hivyo, kuna vighairi vichache vya kategoria hizo visivyokuwa na kiambishi tangulizi, hususan vivumishi viulizi na nomino zinazotaja majina ya ndugu kama vile maha (mama), kaaka (bibi) na guuku (babu). Aidha, imebainika kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika nomino iliyopo kwenye kiima au kiarifu cha tungo hata kama tungo hiyo ina ukanushi, taarifa au ,asharti. Pia, utafiti huu umebaini kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika kielezi kinapoandamana nakitenzi katika tungo. Kadhalika, imebainika kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika nomino iliyopo kabla ya kibainishi kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika nomino iliyopo kabla ya kibainishi kioneshi. Zaidi ya hayo, imenainika kuwa kiambishi tangulizi hakitokei katika nomino iliyopo baada ya kibainishi kioneshi. Vilevile, utafiti huu umebaini kuwa kiambishi tangulizi hutokea kwenye kivumishi cha pekee kinachotanguliwa na nomino. Pia, imebainika kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika nomino iliyotanguliwa na kihusishi, nomino ya uhusika milikishi na nomino iliyotanguliwa na kiunganiishi huru. Utokeaji huu hutokana na michakato ya udondoshaji, uunganishaji na urefushaji wa irabu ya kihusishi, irabu ya kimilikishi au kiunganishi huru kilichotangulia nomino husika. Kwa hiyo, utafiti huu umebaini kuwa mazingira ya kimofolojia na kisintaksia ndiyo huamua kutokea au kutokutokea kwa kiambishi tangulizi katika lugha ya Kisubi. Aidha, utafiti huu umependekeza utafiti mwingine ufanyike katika kipengele cha ulinganishi wa ruwaza za utokeaji wa kiambiishi tangulizi katika lugha mbalimbali za Kibantu au zisizo za Kibantu.swBantu languageKisubiTanzaniaUtokeaji wa kiambishi tangulizi katika lugha ya kisubiThesis