Davison, Monica2022-05-122022-05-122019Davison, M.(2019) Uchambuzi wa takriri ya msamiati katika nyimbo za tamthilia ya nguzo mama (2010),tasnifu ya MA(kiswahili). Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Dar es Salaam.http://41.86.172.12:8090/xmlui/handle/123456789/16596Available in print form, Eat Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library,(THS EAF PN3171D284)Takriri ni kipengele cha ushikamani wa msamiati ambacho kinahusisha marudio ya neno moja, matumizi ya visawe, hiponimu na hipanimu na maneno jumuishi. Utafiti huu unachambua takriri ya msamiati katika nyimbo zilizo katika tamthilia ya nguzo mama (Muhando 2010). Unaonesha jinsi kipengele kimoja katika matini kinavyoweza kuakisi na kuchanuza maana ya matini nzima. Ili kufanikisha kazi hii, nadharia ya ushikamani (halliday na Hassan 1976) na ya mchomozo ( leech 2008) ziliongoza utafiti huu. Mbinu za utafiti zilihusu: usampulishaji lengwa, usomaji makini na uchambuzi wa data kwa njia ya kitakwimu na kitaamuli. Tumebaini kuwa mwandishi alitumia aina zote za takriri ya msamiati ambazo ni takriri ya neno moja, visawe, hiponiumu na hipanimu na maneno jumuishi. Kadhalika, utafii umebaini kuwa takriri ya msamiati iliyotumiwa na mwandishi inawasilisha vizuri msisitizo wa wadhamira, migogoro ujumbe msimamo na falsafa ya mwandishi katika matini tulizochambua ( nyimbo ) kuna mbanano mkubwa wa takriri ya msamiati ambayo ilisababishwa na utokeaji wa alama za takriri ya msamiati zilizotokea kati ya mstari mmoja hadi wa nne. Mbanano huu unaonesha kuwa mwandishi alikuwa na kusudi la kukazia ujumbe wake kwa hadhira. Vilevile kuna ulegelege wa ala za ushikamani kwa kiwango kidogo. Hata hivo ulegelege huo haukuathiri mbanano uliopo katika nyimbo hizi. Kupitia utaii huu tumegundua kuwa takriri katika matini tulivochunguza ni muhimu katika ujenzi wa matini nzima na inauwezo wa kuwasilisha maana au ujumbe wa matini nzima. Tunapendekeza kuwa tafiti zijazo zichunguze takriri katika vipengele vingine vinavojenga tamdhilia hii kama usimulizi na mazungumzo. Vilevile, tafiti zijazo zinaweza kutumia mbinu yoyote ya kielimu-mitindo katika uchambuzi wa kipengele chochote cha matini na kisha kukihusisha na matini kubwa.swSwahili literatureSwahili languageDrama in educationStudy and teachingDramaPlayUchambuzi wa takriri ya msamiati katika nyimbo za tamthilia ya nguzo mama (2010)Thesis