Mzee, Fatma Aboud2020-04-282020-04-282013Mzee, F. A (2013) Maudhui katika nyimbo za taarab za bi Shakila, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.http://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/10452Available in printed form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.S24M93)Lengo la utafiti huu ni kuchunguza nafasi ya maudhui katika nyimbo za taarab za Bi. Shakila yanavyosawiri hali halisi ya jamii. Utafiti huu ulipitia machapisho mbalimbali na data za msingi zilipatikana kwa kufanya usaili na msanii teule Bi. Shakila pamoja na watafitiwa wengine. Data za upili zilipatikana katika maktaba, makumbusho na kwenye mtandao. Nadharia ya semiotiki kupitia misimbo yake kama kihementiki, ishara, kirejelezi, matukio na kiseme ndio iliyosaidia uchambuzi wa data. Matokeo ya utafiti huu yamebaini kuwa nyimbo za Bi. Shakila zimeshamiri dhamira kadha wa kadha. Baadhi yake ni umalaya, ufisadi, umbeya, mmomonyoko wa maadili, dini, malezi bora, umuhimu wa tabia njema, umuhimu wa wazazi, ukombozi, matendo mema, umuhimu wa kuilinda nchi na umuhimu wa mapenzi. Dhamira ambazo zinasawiri maisha halisi ya mwanadamu katika jamii yetu. Matokeo ya utafiti huu pia yamebaini kuwa nyimbo za Bi. Shakila zimetumia matumizi mbalimbali ya lugha ili kufikisha maudhui yaliyokusudiwa kwa hadhira. Hii ni pamoja na kuficha lugha ya matusi ili kuondoa karaha, kuepusha ugomvi na mfarakano miongoni mwa jamii. Matumizi hayo ya lugha ni pamoja na taswira na ishara, tamathali za semi, methali na mafumbo. Hivyo, utafiti huu unatoa maoni kwa watunzi wa nyimbo za taarab kutunga nyimbo ambazo zinazingatia maadili, zinaelimisha, zinaonya na kurekebisha jamii. Maoni na mapendekezo pia yametolewa kwa serikali, watafiti na jamii kwa ujumla.otherSwahili literatureSaid, ShakilaMaudhui katika nyimbo za taarab za bi ShakilaThesis