Mashauri, Michael A.2020-04-032020-04-032012Mashauri, M A.(2012) Toni katika nomino za lugha ya ki-konongo, Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.http://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/8894Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8025.T34M373 )Lugha nyingi za ki-Bantu ni lugha zenye toni (taz. Nurse na Philippson 2003: 8). Pamoja na ukweli huo kubainishwa, na wataalamu mbalimbali kujaribu kuchanganua vipengele vya toni katika lugha za ki-Bantu bado lugha nyingi hazijafanyiwa utafiti wa kutosha na nyingine hazijaandikiwa kabisa. Miongoni mwa lugha ambazo hazijaandikiwa ni lugha ya ki-Konongo. Hivyo basi, utafiti huu unahusu toni katika nomino za lugha hii katika kujaribu kuziba pengo hili. Data zilizotumika katika utafiti huu ni nomino zilizokusanywa uwandani katika kijiji cha Inyonga na Mtakuja tarafa ya Inyonga, Wilayani Mlele, Mkoa wa Katavi. Data zilikusanywa kwa hojaji, mahojiano na kurekodiwa kwa kinasasauti aina ya MP3 IC recorder na kuchambuliwa kwa mbinu ya uchanganuzi wa data kimada. Katika uchanganuzi wa data tumetumia nadharia ya Fonolojia Vipandesauti Huru iliyoasisiwa na Goldsmith (1976) ambapo vipengele vya kifonolojia vimewakilishwa katika rusu huru. Utafiti huu umegusia vipengele vya kifonolojia kama vile irabu, konsonanti, silabi na michakato ya kifonolojia inayoathiri toni. Aidha, tumezungumzia vipengele vya kimofolojia vinavyogusa kipengele cha toni kama vile uradidi na mwambatano wa nomino. Imebainika pia lcuwa toni za lugha hii ni tabirifu na huwa na kiinitoni lcinachopachikwa katika kiambishi awali kitangulizi kwa mashina ya nomino yasiyo na kiinitoni; yaani nomino za ngelitoni ya I; katika ngelitoni ya II kinapachikwa katika kiambishi awali kitangulizi na silabi ya mwisho kasoro moja na zile za ngelitoni ya III na IV kiinitoni kinapachikwa katika kiambishi awali kitangulizi na silabi ya mwisho ya shina. Kwa upande wa viambishi ni kiambishi awali kitangulizi na viambishi vya mahali pekee ndivyo vyenye kiinitoni na huwa na tonijuu. Vilevile kuna kanuni kadhaa ambazo zimejibainisha kama vile upachikaji kiinitoni, usambaaji tonijuu ya mwisho, ushukajitoni kihatua, upandaji tonichini, uundaji tonipanda au tonishuka na kanuni za uhusishaji KTM na kiinitoniotherKonongo language,Bantu languagesToneNounToni katika nomino za lugha ya ki-konongoThesis