Mhando, Chiku Jumanne2020-04-012020-04-012012Mhando, C J (2012) Nafasi ya maana ya dhima katika uainishaji wa nomino za kibantu data toka ki-bondei,Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaamhttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/8672Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8081.M4752 )Utafiti huu unahusu nafasi ya maana/dhima /a uainishaji wa nomino za Kibantu data toka Ki-Bondei. Ki-Bondei ni lugha ya Kibantu inayo/ungumzwa Kaskazini- Magharibi mwa mkoa wa Tanga nchini Tanzania. Jumla ya watafltiwa 40 kutoka katika kijiji cha Kibanda, kijiji cha Semngano, Kijiji cha Kivindo na Kijiji cha Kwasemnyau walitumiwa, uteuzi wao ulikuwa wa kinasibu. Taarifa zimekusanywa kwa watafltiwa kwa njia ya hojaji, mahojiano na ushuhudiaji. Utafiti huu ulikuwa na malengo yafuatayo: kubainisha ngeli za Ki-Bondei na idadi yake kwa kutumia msingi wa kimofolojia na kufafanua dhima mbalimbali zinazojitokeza katika viambishi ngeli vya nomino.Mkabala wa Viambishi Awali vya Nomino ulitumika kwa nia ya kutimiza malengo haya. Mkabala huu wa Viambishi Awali vya Nomino umetumika ili kubainisha viambishi ngeli vya nomino katika misingi ya umoja na wingi. Katika uchunguzi wetu tumebaini kuna ngeli 19 za Ki-Bondei. Pia utafiti huu umebaini kuwa katika lugha ya Ki-Bondei, viambishi ngeli vya nomino vina dhima kama vile umoja/wingi, ukubwa/udogo na uzuri/ubaya. Dhima zote hizi huweza kujitokeza katika kiambishi kimoja kwa wakati mmoja hali Ambayo husababisha kutokea kwa utata.otherkiswahili languagekibantuKi-BondeiNafasi ya maana ya dhima katika uainishaji wa nomino za kibantu data toka ki-bondeiThesis