Mahenge, Elizabeth Godwin2021-10-062021-10-062019Mahenge E.G (2019) Uumbaji Wa Ualbino Katika Fasihi Ya Kiswahili; Uchambuzi Wa Kazi Teule,Tasnifu ya uzamivu,Chuo kikuu cha Dar es salaamhttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/15859Available in print form,East Africana Collection ,Dr.Wilbert Chagula Library,Class mark ( THS EAF PL8704T34M333)Utafiti huu ulihusu uchambuzi wa kazi teule katika fasihi ya Kiswahili ili kuona namna uumbaji wa albino unavyofanyika. Utafiti ulikuwa na malengo mahsusi manne ambayo ni kubainisha imani zinazoumba ualbino katika kazi teule za fasihi ya Kiswahili; kuelezea dhima ya msimulizi zinazotumiwa kuumba ualbino katika kazi teule.Utafiti ulihusisha kazi nane za fasihi ya Kiswahili ambazo ni Takadini, Nje Ndani, Zindera, Baba Ne-Musa “Mimi Albino”, Wimbo wangu Albino”, “Albino” na “Mauaji ya Albino,” Mbinu ya uchambuzi wa nyaraka ilitumika ili kupata matokeo ya utafiti huu. Mbinu hii ya uchambuzi wa nyaraka ilitumika ili kupata matokeo ya utafiti huu. Mbinu hii ya uchambuzi iliongozwa na Nadharia ya Naratolojia. Nadharia hii inahusika kuchunguza namna usimulizi unavyofanywa katika simulizi.Utafiti unafuata mkabala wa Bal ambao unaona kuna usimulizi kaitika kila kitu. Data zilipatikana baada ya kusoma kwa kina kazi teule pamoja na kufanya mahojiano kwa ajili ya utafiti wa awali wa utafiti huu. Mkabala uliotumika katika uchambuzi wa data ni wa kitaamuli ambao ni wa kimaelezo na uliwezesha kupatikana kwa matokeo ya utafiti huu. Kwanza , utafiti umebaini kuwa kuna imani mbalimbali zinazoelezea asili ya kuzaliwa motto mwenye ualbino. Imani hizi zinatokana na visasili vilivyopo katika jamii.Pili, utafiti umebaini kuwa , msimulizi anatumia tamathali za usemi ili kuumba ualbino kiubaguzi na kiunyanyapaa kwa upande mmoja; na pia anatumia tamathali za usemi ili kuumba ualbino kiujumuishwaji kwa pande mwingine.Tatu, utafiti umebaini kuwa msimulizi anajititokeza kwa dhima ynne ambazo ni kusimulia kuwasiliana, kukosoa na kutekeleza itikadi. Katika dhima hizi, msimulizi anawezakuwa hai (akishiriki katika kusimulia) au tuli( akijenga kusimulia), Nne, utafiti umebaini kuwa , sauti za usimulizi zinatumika kwa makusudi maalum ambayo ni ama kuunga knono jambo Fulani au kulipinga. Matumizi ya nafi ya kwanza nay a pili yanaonesha kuunga mkono jambo; wakati matumizi ya nafsi ya tatu yanaonesha kulipinga. Mapendekezo yanayotolea na utafiti huu ni kufanya utafiti mwingine katika kumbo mahususi za fasihi ili kuona namna ualbino kwa umahususi na ulemavu kwa ujumla unavyoumbwa katika kumbo hizo Vilevile utafiti unapendekeza nadharia ya Naratolojia itumiwe zaidi na wachambuzi wa kazi za kifasihi kwa kuwa inamwezesha mchambuzi kuufahamu uhalisia wa simulizi kupitia nafsi mahususi zinazotumika katika kusimulia.Nadharia hii iko karibu na uhalisia.swLanguage and languagesSwahili languageSwahili literatureAlbinos and albinismTanzaniaUumbaji Wa Ualbino Katika Fasihi Ya Kiswahili; Uchambuzi Wa Kazi TeuleThesis