Sway, Neema Benson2021-10-112021-10-112015Sway, N. B. (2015) Dhima ya korasi katika utendaji wa ushairi simulizi mifano kutoka tamasha teule la nyimbo za bongo fleva la msanii nasibu abduli “diamond”. tasnifu ya MA(kiswahili). Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Dar es Salaam.http://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/15939Available in print form, Eat Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library,(THS EAF PL8703.5.S92)Tasinifu hii ililenga katika kuchunguza dhima ya korasi katika utendaji wa ushairi simulizi kupitia tamasha teule “Diamonds are Forever” la nyimbo za bongo fleva la msanii Nasib Abdul “Diamond”. Malengo mahususi yalidhamiria kufafanunua vipengele vya korasi vya kifani na vya kiamudhui kupitia uttendaji wa nyimbo izo, kisha kueleza dhima ya vipengele hivyo katika kukamilisha utendaji wa ushairi simulizi. Utafiti huu katika ukusanyaji wa data, umetumia mbinu ya kusoma maandiko maktabani, utazamaji wa nyimbo zilizo rekodiwa, mahojiano, hojaji na majadiliano ya wasanii, madijei, wanafunzi na umahiri (M.A Kiswahili Fasihi) na wadau wa muziki wa bongo fleva wa mtandaoni na mashabiki wa huu. Nadharia ya Korasi iliyoasisiwa na Mutembei (2012) ndiyo iliotumika katika uchambuzi wa data za utafiti huu pamoja na mbinu ya kitaamuli. Matokeo ya utafiti kwa upande wa fani yamedhihirisha kwamba katika utendaji wa nyimbo za bongo fleva korasi inaweza kujitokeza , mathalani, kama mhusika (mhusika mkuu, mhusika kiungo, ahusika ambatani na wahusika watazamaji), kama kiitikio, mkarara, kimya, muundo, na mtindo (matumiziya giza, simulizi na mazungumzo mwanzo wa onesho na matendo bubu) ambao huweza kuwa ni wa kiparodosi (kitangulizi) au kiukengeushi. Vilevile, korasi katika utafiti huu imejitokeza kama falsafa na kama dhamira. Vipengele hivi vimekua ni mhiliwa utokeajii wa kazi nzima ya kisanaa ambapo kwavyo maadili ya jamii yameweza kupimwa na kuegemezwa. Kwa ujumla vipengele vya korasi kifani na kimaudhui vimesaidia kukamilisha utendaji wa ushairi simulizi kwa; kuhamasisha ushirikishwaji wa hadhira, kuchochea hisia za hadhira, kuibua fikra za hadhira, kudokeza na kusisitiza maudhui ya kazi ya fasihi kwa hadhira, kujenge mshikamano thabiti wa kazi ya sanaa, kutambulisha upekee wa msanii, kuvuta usikivu na umakini wa hadhira, na kuimarisha utendaji wa fanani kwa ujumla.swSwahili literatureDhima ya korasi katika utendaji wa ushairi simulizi mifano kutoka tamasha teule la nyimbo za bongo fleva la msanii nasibu abduli “diamond”Thesis